Monday, February 28, 2011

Harambee ya kuchangia maafa ya Gongo la Mboto iliyofanyika London








Salaam,

Tunapenda kutoa shukrani zetu za Dhati kwa watanzania wote  waishio LONDON UK walioweza kufika jana jioni AFRICAN VILLAGE BAR & RESTAURANT kuchangia waathirika wa Gongo la Mboto Tanzania. Kwa mda wa masaa mawili  

tumeweza kukusanya Jumla ya  pesa taslim Pounds £600, pia tumekusanya Nguo nyingi kutoka kwa watu mbalimbali na vifaa vingine mbali mbali. 

Ningependa kutoa shukrani za dhati kutoka URBAN PULSE,MISS JESTINA BLOG,AIL TV, LOCUS IMPEX SHIPPING CO, SHILLA FRISCH, NA Utawala wa AFRICAN VILLAGE BAR & RESTAURANT LONDON kwa kusaidia na kuwezesha kufanikiwa kwa zoezi la jana.

Mungu Ibariki Africa, Mungu Ibariki Tanzania
Asanteni

No comments: