Jihadhari na kirusi cha kompyuta -
Akaunti nyingi za mishahara za wateja kadhaa hapa Norway, zimeshambuliwa na kirusi vya kompyuta kiitwavyo “SpyEye”. Kirusi hiki kinajificha kwenye "system" ya kompyuta yako, na wakati ukigonga "username" na nywila, basi kinaiba vyote viwili. Waliotuma kirusi hiki wanapata "access" ya akaunti yako na ndipo wanapoanza kukuibia. Wezi hawa ni wajanja, kwani hawachukui hela nyingi kwenye akaunti moja, bali wanachota kidogo kwenye akaunti nyingi. Jana mchana Kitengo cha mabenki kinachohusika na uhakiki wa mabenki (Bankenes Standardiseringskontor, BSK ) na Jumuiya ya wafanyakazi wa mabenki, bima na taasisi za kifedha (Finansnæringens fellesorganisasjon, FNO = Finance Norway), benki ya Nordea na DnB NOR wametoa taarifa ya kuwaonya wateja wa mabenki kuwa waangalifu na akaunti zao.
Wateja wameombwa kufuatilia akaunti zao kwa makini na kutoa taarifa haraka kwenye mabenki yao, punde tu watakapoona kuwa kuna walakini kwenye akaunti zao. Wateja wote wanaotumia kompyuta, kwenye kuingiza na kutoa pesa, wameombwa kuhakikisha kuwa wanakuwa na “Anti-virus” na “Malware Cleaner” zilizokuwa “updated”.
No comments:
Post a Comment