Wednesday, February 23, 2011

Oslo, Norway

Wageni wanaoishi kihalali kupewa vitambulisho vyenye alama za vidole


Wizara ya sheria hapa Norway, imependekeza kuwa wageni wote wanaoishi kihalali hapa na ambao wametoka nje ya nchi za EFTA (European Free Trade Association) wapewe vitambulisho vitakavyokuwa na jina, namba za taifa (National Identity Number/fødselsnummer) ambazo hutolewa kwa wote waishio hapa Norway, picha na alama za vidole zitakazokuwa kwenye “chip”.

Lengo la vitambulisho kwa wageni waishio kihalali ni kuhakikisha kuwa kunakuwa na urahisi wa kuwatambua wageni waishio kinyume cha sheria.

Hii inafuatia shinikizo kutoka kwenye Umoja wa Ulaya (EU) ambayo Norway si mwanachama, lakini nchi za EFTA zina makubaliano na EU kuhusu kuingia kwa wageni kwenye nchi za Ulaya; yaani makubaliano ya Schengen.

Chanzo cha habari: Aftenposten Jumatano 23.02.2011 ukurasa wa 6.

1 comment:

Anonymous said...

JAMANI ASANTENI KWA TAARIFA HIZI. NAONA BORA NICHUKUE URAIA KUEPUKANA KUTEMBEA NA KITAMBULISHO KILA KUKICHA.