Tuesday, March 15, 2011



Bunge la Norway (Stortinget)
lakataa kupiga marufuku uvaaji wa
hijab mashuleni.


Bunge la Norway leo hii limekataa kupitisha mswada kutoka Fremskrittspartiet (Progressive Party) wa kupiga marufuku uvaaji wa hijab mashuleni. Bunge limetoa mapendekezo yake kwa kusema kuwa, mwalimu anaweza kumlazimisha mwanafunzi aweke hijab yake kiasi ambacho sura ya huyo mwanafunzi ionekane vizuri. Mashule yameachiwa kuzungumzia na kujiwekea visheria kuhusu suala la hijab, niqab na burka wakishirikiana na wazazi wa wanafunzi wanaovaa mavazi hayo.

No comments: