Tuesday, March 15, 2011

Daktari: Mgonjwa wa Loliondo amepona UKIMWI!!!


Wagonjwa wa magonjwa mbalimbali wakipewa dawa na Babu Mchungaji wa Loliondo.

DAKTARI Joachiam Mbosha wa Hospitali Teule ya Wilaya ya Ngorongoro ya Wasso, amethibitisha kuwa mmoja wa wagonjwa wa Ukimwi aliyekwenda kutibiwa kwa Mchungaji Ambilikile Mwasapile, maarufu kwa jina la 'Babu', huko Samunge, Loliondo amepona Ukimwi.
Wilia John Lengume (30), juzi alikuwa kivutio kwa mamia ya watu baada ya kutangazwa na Mchungaji Mwasapile kwenye ibada iliyofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT), Usharika wa Sonjo iliyoshirikisha mamia ya watu. Akizungumza katika ibada hiyo, Mchungaji Mwasapile alisema Lengume ndiye aliyekuwa mgonjwa wa kwanza kumtibu.



No comments: