Friday, April 27, 2012

CHAMA CHA WATANZANIA SWEDEN


(TANZANISKA RIKSFÖRBUNDET)
Kwa watanzania pamoja na marafiki!

Kamati ya muda iliyoteuliwa Ubalozini kwa nia ya kuanzisha chama cha watanzania Sweden inawakaribisha katika hafla fupi yaufunguzi wa chama na pia kuchagua viongozi watakaondeleza shuguli za chama.

Mgeni wa heshima katika ufunguzi na uchaguzi wa viongozi wa Chama cha Watanzania atakuwa Mh. Balozi Muhammed Mwinyi Haji Mzale.

Sehemu: Tanzania house, Näsby Allè 6, Täby

Tarehe na Wakati: Tarehe 28 Aprili 2012: Saa tisa mchana mpaka saa kumi na moja jioni (saa 9 mchana - 11 Jioni).

Atakayependa kugombea uongozi ajaze fomu ya kujiandikisha kugombea uongozi wa chama na kuituma kwa katibu kwa anuani pepe kama inavyoonekana hapo chini.

Wote mnakaribishwa na ukipata taarifa hii tafadhali mtumie na mwingine!

Kamati ya wanamchakato kupitia

Katibu wa Muda

Bi. Angela Wilberd:
tanzanianswe@hotmail.com 

No comments: