Monday, May 07, 2012

Blogu ya CCM iko hewani


Chama Cha Mapinduzi kupitia kitengo cha Mawasiliano na Umma chini ya Idara ya Itikadi na Uenezi imeanzisha Blogu ambayo pamoja na kuhabarisha habari za mapema kabisa za shughuli za Chama, lakini itakuwa ikiyapa kipaombele pia kuhabarisha matukio mbalimbali tangu ya Kijamii, Siasa, Biashara, Uchumi, Burudani, Sanaa na Michezo na pia kupokea na kuyasambaza maoni ya wengine ili mradi yatakuwa na lengo linalotofautiana na ukiukwaji wa maadili ya vyombo vya habari.

Kwa heshima, Chama Cha Mapinduzi kinawasilisha kwako uitangaze Blogu hii kama utakavyoona inafaa, lakini pia uendelee kuanzia sasa kuwa mdau wa kuiperuzi ili kuwa chanzo chako cha kwanza cha kupata habari muhimu za kitaifa na kimataifa.

Baadhi ya dondoo muhimu kuhusiana na blogu hii zipo kwenye Logo iliyoambatanishwa na salam hizi.

Blog: www.ccmchama.blogspot.com 

No comments: