Ubaguzi wa rangi katika sanaa Ulaya
Kwa shindano linalolenga kusherehekea
usanii wa kitsch (barani Uropa), shindano la muimbaji bora la Eurovision kila
linapofanyika huzua hisia za kichochezi ambazo sio kawaida kutokea kwingineko.
Na hivyo ndivyo ilivyo mwaka huu wakati shindano hilo likielekea
kileleni. Hisia za ubaguzi wa rangi tayari zimeanza kuzungumziwa kabla ya
shindano hilo kufika fainali.
Chama chenye msimamo mkali cha Freedom Party, nchini Ukrain,
kilimshambulia kwa maneno msanii Gaitana - ambaye ni mzaliwa wa Congo na ambaye
anawakilisha Ukraia kwenye shindano hilo.
"Mamilioni ya watu watakaokuwa wanatizama fainali ya
shindano hilo, watajionea Ukraian ikiwakilishwa na mtu ambaye sio wa rangi
yetu" ndivyo alivyosema Yuri Syrotyuk, ambaye chama chake kianajiandaa kwa
uchaguzi wa wabunge baadaye mwaka huu.
"Ukrain itaonekana kama nchi iliyo katika eneo la vijijini
huko barani Afrika" aliongeza kusema Yuri Syrotyuk,
Shutuma
Hata hivyo baadaye alikana madai ya ubaguzi wa rangi, akisema
kuwa alikuwa anakosoa tu kutokuwepo uwazi katika namna mwakilishi kutoka nchini
humo alivyochaguliwa.
Lakini matamshi yake yalikemewa sana nchini Ukraine na vyama
vyote rasmi vya kisiasa na wasanii wengine mfano Vitaly, Volodymyr Klitschko na
mshindi wa shindano hilo mwaka 2004, Ruslana.
Gaitana, atamenyana na wenzake katika awamu ya nusu fainali
Alhamisi usiku, na amesema kuwa matamashi hayo ya ubaguzi wa rangi yameonyesha
tatizo hilo lilivyokithiri nchini Ukraine.
"Nimekerwa sana na matamshi hayo, kwa sababu Ukrain ni nchi
yenye demokrasia ambako watu wenye unyenykevu na utu wanaishi" alisema
Gaitana.
Tamaduni mbili
Babake Gaitana ambaye ni raia wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya
Congo, alisomea katika mji mkuu wa Ukrain, Kiev, ambako alikutana na mamake
Gaitana na kumuoa.
Muda mfupi baada ya kuzaliwa kwa Gaitana, mwaka 1979, familia
yake ilihamia Congo-Brazzaville ambako waliishi kwa miaka mitano. Hata hivyo
wazazi wake walitalakiana lakini mamake Gaitana alirejea naye nchini Ukrain.
Gaitana huandika nyimbo zake mwenyewe na anajioana kama
mchanganyiko wa tamamduni mbili kwa sababu marafiki zake nchini Congo wansema
mziki wake una mizizi ya Kiafrika.
Fainali ya shindano hilo itafanyika nchini Azerbaijan na
kutazamwa na watu milioni 125 kote barani Uropa. Wengi wanaona
kama Gaitana ana nafasi nzuri ya kushinda shindano hilo.
Atamenyana na washindani kutoka nchini
Sweden, Uturuki, Romania, Italia na Ugiriki.
BBC Kiswahili www.bbcswahili.com
No comments:
Post a Comment