Rais wa Ghana John Attah Mills afariki
Rais wa Ghana
John Atta Mills amefariki ghafla wakati akipata matibabu.
Taarifa kutoka afisi ya rais zinasema
kuwa alifariki ghafla baada ya kupelekwa hospitali siku ya Jumatatu usiku.
Msaidizi wake pia amethibitisha kufariki
kwa kiongozi huyo. Kifo cha rais wa taifa la pili duniani kwa ukuzaji wa cocoa
kimekuja wakati alikuwa anajiandaa kupogania tena urais. Wakati wa uongozi
wake, uchumi wa Ghana uliimarika na demokrasia kupanuka zaidi.
"Ni kwa masikitiko makuu na kwa
moyo mzito... Tunatangaza kifo cha ghafla cha rais wa jamhuri ya Ghana "
taarifa iliyotumiwa shirika la Reuters kutoka ofisi ya rais ilisema.
Tarifa hiyo ilisema kuwa Rais Mills
mwenye umri wa miaka 68 alifariki saa chache tu baada ya kupelekwa hospitali. Hata hivyo hakuna maelezo zaidi
yaliyotolewa.
Lakini msaidizi wake mmoja ambaye
hakutaka kutajwa, alisema kuwa Rais John Attah Millis alisikika siku ya
Jumatatu akilalamika kwa anaumwa.
Hali yake ilizorota na hatimae kufariki
mapema siku ya Jumanne.
Mills, anajulikana kwa kuanzisha
uchimbaji wa mafuta nchi Ghana.
Chanzo: BBC Kiswahili
No comments:
Post a Comment