Taarifa kwa Baraza la Wawakilishi juu ya
usajili wa meli za nje uliofanywa na SMZ kupitia Mamlaka ya Usafiri Baharini
Zanzibar “Zanzibar Maritime Authority –ZMA”
Waziri wa Zanzibar Bandari Mawasiliano na Ushukuzi Hamadi Masoud Hamadi.
Mhe.
Spika,
Tarehe
27/06/2012 Vyombo vya Habari hapa Tanzania (The Citizen) na nchi za nje
(International news Agency – Bloomberg) viliandika makala kuhusu usajili wa
meli 10 za mafuta (Tankers). Ilidaiwa katika makala hayo kuwa Meli hizo
zilisajiliwa Zanzibar na zinapeperusha Bendera ya Tanzania na kwamba zinafanya
biashara na Kampuni ya Serikali ya IRAN.
Gazeti la
“The Citizen la tarehe 27 Juni, 2012 lilikuwa na kichwa cha habari “Iran
Tankers adopt TZ Flag to avoid embargo” (meli za mafuta za Iran zinatumia bendera
ya Tz kukwepa vikwazo.
TAARIFA YA
ZMA
Mamlaka ya
Usafiri Baharini Zanzibar Maritime Authority – ZMA ni Mamlaka iliyoundwa kwa
sheria No. 3 ya mwaka 2009 ambayo pamoja na kazi nyengine inasimamia
utekelezaji wa Sheria ya usafiri wa Bahari Zanzibar ya mwaka 2006 (Zanzibar
Maritime Transport Act 2006).
Sheria
ya Zanzibar Maritime Transport Act 2006, kifungu no. 8 cha sheria hii,
kinasomeka kama ifuatavyo:
(a).
Tanzania Zanzibar International Register of Shipping for ocean going ships;
and
(b) Tanzania
Zanzibar Register of Shipping for coastal Ships.
(2). A
ship shall be a Tanzania Zanzibar ship for the purpose of this Act if that ship
is registered under this part.
Katika
kutekeleza jukumu la usajili wa meli kama ilivyoelekezwa katika kifungu 8(1)(a)
hapo juu, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imetiliana mkataba na kampuni ya
PHILTEX ya Dubai kufanya usajili wa meli za kimataifa. (Open Registry).
Usajili huu
umekuwa ukifanyika tangu mwaka 2009 na mpaka sasa ZMA kupitia Wakala wake
imesajili meli 399 ikiwa ni pamoja na meli za mafuta, makontena, General cargo
na meli za Abiria.
Kama
nilivyoeleza hapo awali, vyombo vya habari vimechapisha makala ya usajili wa
meli 10 ambazo zinadaiwa ni meli za IRAN kulingana na makala zao hizo.
SMZ
inatoa taarifa rasmi juu ya meli za mafuta ilizosajiliwa wiki mbili zilizopita
pamoja na majina ya meli, ukubwa wake, majina ya makampuni inayomiliki meli
hizo na nchi zilizotoka kabla ya kupata usajili kwa ZMA, kama ifuatavyo:
Jina
la meli GRT (Ukubwa) Company name Ilikotoka
1.
Daisy 81479 Daisy Shipping Co. Ltd Malta
2. Justice
164241 Justice Shipping Co. Ltd Cyprus
3. Magnolia
81479 Magnolia Shipping Co. Ltd Malta
4. Lantana
81479 Lantana Shipping Co. Ltd Malta
5.
Leadership 164241 Leadership Shipping Co. Ltd Cyprus
6. Companion
164241 Companion Shipping Co. Ltd Malta
7.
Camellia 81479 Camellia Shipping Co. Ltd Malta
8.
Clove 81479 Clove shipping Co. Ltd Malta
9. Courage
163660 Courage Shipping Co. ltd Cyprus
10. Freedom
163660 Freedom shipping Co. Ltd Cyprus
11. valor
160930 valor Shipping Co. Ltd. Cyprus
Jumla
ya GRT ni 1,388,368 tons Meli hizi ni 11 kama zinavyoonekana katika orodha hapo
juu ni miongoni mwa meli nyingi zinazobadilisha usajili wao (De
registration).
Meli
zilizosajiliwa na ZMA zinatoka nchini Cyprus na Malta. Sambamaba na meli hizi
11 zilizosajiliwa na ZMA, meli za mafuta nyengine 20 ambazo zinasemekana
zilikuwa kwenye usajili wa nchi za Ulaya zimebadilisha usajili wao na kwenda
usajili wa “TUVALU Islands”.
ZMA
ilimtaka Wakala wake Philtex Corporation kuwaita wenye meli hizi na kuwataka kujieleza
kuhusu uhusuiano wao na Serikali ya au makampuni ya mafuta ya IRAN.
Philtex
ilikutana na Wamiliki hao siku ya Alkhamis tarehe 28/06/2012 katika afisi za
Philtex Corporation na Wamiliki hao wameeleza kwamba hawana uhusianao na
Serikali au mamlaka yoyote nchini Iran na wameamua kuja kusajili meli
ZMA kwa
ridhaa yao na kwa kufata matangazo ya usajili wetu wa nje (Open Registry).
Pamoja na maelezo hayo, wamiliki hao wametangaza kwamba ikiwa ZMA haiko tayari
kuendelea na usajili wa meli zao, wanaweza kufuta usajili wao na tayari
wanafikiria kufanya mazungumzo na open Registry nyengine (PANAMA) lakini hawana
nia ya kurudi walikotoka, yaani Cyprus na Malta.
Kinyume
na maelezo yaliyotolewa na vyombo vya habari juu ya uraia wa wamiliki wa meli
hizi, Wamiliki wa meli hizi kama walivyojieleza katika usajili wa meli zao wana
uraia wa British Vergin Islands na Sychelles. Kulingana na “United Nations
Convention Law of the Sea”, Article 91, na za “Geneva convection of
Registration” articles 6, 7 na 8, na kulingana na Zanzibar Maritime Transport
Act of 2006, section 8, Zanzibar ikiwa ni nchi moja kati ya nchi mbili
zinazounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayo haki ya kusajili meli yeyote
kulingana na taratibu na Sheria za Zanzibar, na sheria za Kimataifa
zinazoongoza usajili huo.
Maelezo
haya yanatolewa ili kutoa usahihi wa uvumi kuwa Zanzibar imesajili meli za IRAN
ambazo zimewekewa vikwazo na Marekani na nchi za Umoja wa Ulaya (European
Union) juu ya usafirishaji na uuzaji wa mafuta kutoka Iran.
Mhe.
Spika, taarifa hizi za vyombo vya habari hazina madhumuni yeyote zaidi ya
kuwavunja moyo wenye Makampuni ya meli wanaotaka kusajili meli zao kwetu.
Hivyo
basi Serikali inatamka wazi kwamba Usajili uliofanywa kwa meli hizi umefuata
taratibu zote zilizowekwa kisheria na kwamba Serikali imekuwa ikifanya na
itaendelea kufanya mazungumzo na wenye meli mbalimbali ili kuongeza idadi na
ukubwa wa meli inazosajili nje ya nchi.
Biashara hii
ya ukubwa wa GRT 1,388,368 Tons katika kipindi cha wiki mbili na maombi mapya
matano kwa meli zitakazokuwa na ukubwa wa zaidi ya GRT 500,000 imeshtua
Makamuni mengine na hata nchi nyengine zisizoitakia mema Zanzibar katika juhudi
zake za kukuza mapato na uchumi wake.
Hata
hivyo mamlaka itafata sheria zote zilizowekwa kitaifa na kimataifa katika
biashara ya usafiri baharini na itahakikisha meli zinasajiliwa chini ya mamlaka
hii zinafata taratibu ilizoweka.
Mhe.
Spika, kabla ya taarifa hizi za vyombo vya habari (The Citizen), Waziri wa
Uchukuzi wa SMT Mhe. Harisson Mwakyembe) alipokuwa akijibu suala Bungeni hivi
juzi hakuonyesha kurishiki kwake katika usajili wa meli (Open Registry)
inayofanywa na Zanzibar na kuahidi kufanya ziara ya kuja Zanzibar kuonana na
Waziri anaehusika kuzungumzia suala hili.
Taarifa za
“The Citizen” zaweza kuwa ni muendelezo wa Mhe. Mwakyembe kutoridhika kwake
katika usajili unaofanywa na Serikali kupitia uwakala wake huko Dubai. Mhe.
Spika, Zanzibar haifungiki kusajili meli za nchi yeyote.
Hili ni
suala la kibiashara na kwamba kwa Serikali yetu ni njia moja ya kuongeza mapato
yanayoendesha Serikali, alimradi tu usajili huo hauvunji sheria za
Kimataifa.
Mhe.
Spika, Zanzibar ina uhusiano mkubwa na wa muda mrefu na nchi nyingi ikiwemo
IRAN na hivi karibuni Zanzibar ilipata ugeni (Makamo wa Rais wa Iran) na
viongozi wetu walifanya mazungumzo ya namna gani IRAN itaendelea kusaidia
Zanzibar katika miradi ya Maendeleo.
Zanzibar haingependa
kuingizwa kwa visingizio vyovyote na kwa njama zozote katika migogoro
isiyowahusu. Hivyo, kwa taarifa hii, Serikali inakanusha rasmi uvumi wa vyombo
vya habari kuhusiana na suala hili kama taarifa hii ilivyofafanua hapo juu.
Mhe. Spika, naomba kuwasilisha.
Hamad Masoud Hamad
WAZIRI WA MIUNDOMBINU NA MAWASILIANO ZANZIBAR
No comments:
Post a Comment