Jumuia ya Watanzania; Norway, Sweden, Finland na
Denmark
YAH: HIFADHI YA
JAMII KWA DIASPORA (WESTADI).
Kwa Jumuia ya Watanzania,
Ubalozi wa Tanzania, Sweden, umepokea barua kutoka Wizara yetu ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ikitufahamisha kuhusu kuanzishwa kwa
huduma ya HIFADHI YA JAMII KWA WATANZANIA WAISHIO NJE – Welfare Scheme
for Tanzanians in the Diaspora (WESTADI).
Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) sasa imepanua huduma zake kwa
Watanzania wanaoishi nje ya nchi kupitia Mpango wa Hifadhi ya Jamii kwa
Watanzania waishio ughaibuni (Diaspora). Lengo la bima hii ni kuondoa adha
kubwa inayoipata Diaspora kuhudumia ndugu wanapougua Tanzania, au diaspora
anpougua akiwa likizo Tanzania na Mtanzania anapofariki akiwa nje ya nchi.
Chini ya WESTADI, mwanachana atatakiwa kulipa ada ya dola za Kimarekani
mia tatu (USD 300) kwa mwaka ili kupata mafao kama ifuatavyo;
1. Huduma va matibabu kwa wategemezi wanne (4)
wa Mwanachana ambao wanaishi nyumbani (Tanzania);
2. Huduma ya matibabu kwa Mwanachama pindi
atakaposafiri kuja Tanzania wakati wa likizo au kwa sababu zozote zile;
3. Huduma za kusafirisha mwili wa Mwanachama
kuja nyumbani iwapo atafariki akiwa nje ya nchi pamoja na kulipia tiketi ya
msindikizaji mmoja.
4. Hudurna ya mazishi katika nchi anayoishi
Mwanacharna ikiwa amechagua kuzikwa nchi aliyopo.
Mtegemezi atachagua hospitali iliyo ndani ya
mkoa husika na huduma kwake zitaanza mara moja baada ya kuthibitishwa kwa
ingizo la pesa za Bima ya Mtu aliyeko nje.
Huduma zitasimama mara punde mwenye bima atakapositisha na kuondoa
michango ya pesa za kila mwaka.
Ili kufahamu zaidi juu ya suala hili tafadhali rejea taarifa ya
uzinduzi wa WESTADI uliofanyika Septemba 2011 wakati wa Kongamano
lililoandaliwa na Watanzania waishio, Dikota, Marekani bofya (HAPA).
Mgeni wa heshima katika uzinduzi huu alikuwa Mh. Rais Jakaya Mrisho
Kikwete.
Maelezo zaidi juu ya Mfuko huu na namna ya kuwa mwanachama yako katika
tovuli ya NSSF (http://www.nssf.or.tz).
Ubalozi unaomba muisambaze taarifa hii kwa jumuia ya watanzania na muwasihi wawafahamishe na wengine.
UBALOZI WA TANZANIA,
Näsby Allé 6
|
183 55 Täby
|
Simu: +46 8 732 24 30/31
Fax: +46 8 732 24
32
Baruapepe: mailbox@tanemb.se
Tovuti: http://www.tanemb.se/
SWEDEN
No comments:
Post a Comment