Wednesday, August 29, 2012

Royal Norwegian Air Force Airshow in Oslo this weekend

Jeshi la anga la Norway lasherehekea miaka 100:
Wikiendi hii ndege za kivita kufanya maonyesho Oslo

Major Eskil Amdal of Royal Norwegian Air Force with his F-16 AM (Fighting Falcon) flying over Oslo. The video by Royal Norwegian Armed Forces.


Royal Norwegian Air Force F-16 Display Pilot, Major Eskil Amdal at Kjevik Bernt Balchen Airshow 12.05.2012


Jeshi la anga la Norway (Det norske luftforsvaret) linasherehekea miaka 100 mwaka huu. Limekuwa likifanya maonyesho ya ndege za kivita kuanzia mwezi Mei mwaka huu kwenye miji na sehemu mbalimbali hapa Norway. Wikiendi hii ni zamu ya Oslo. Wananchi wanaombwa samahani kwa makelele yatakayofanywa na ndege hizo.



Ijumaa, 31.Agosti 2012 saa 16:30-17:30  ndege za kivita zitafanya mazoezi kwenye anga la Oslo. Kwenye maonyesho haya kutakuwepo na timu ya akrobatiki ya ndege za kivita ya jeshi la anga la Ufaransa (Patroille Acrobatique de France)


Jumamosi, 01.09.2012  ndio siku rasmi ya maonyesho kwenye anga maeneo ya Halmashauri ya mji wa Oslo (Oslo Rådhus) kukiwa pamoja na ndege za kivita za jeshi la anga la Norway za aina ya F-16 (Fighting Falcon) na za aina ya Alpha za Patroille Acrobatique de France

Jumapili , 02.09.2012 Maonyesho ya jeshi la anga la Norway, Halmashauri  ya mji wa Oslo (Oslo Rådhus).

Maelezo kwa Kiingereza (Information in English): http://mil.no/organisation/news/currentaffairs/Pages/NMA-100-years.aspx


na Mwamedi Semboja

No comments: