Kampuni ya mawasiliano ya
Vodacom Tanzania imekuwa na taarifa na malalamiko
mbalimbali kuhusiana na mauzo ya
vocha ya Tsh450 inayouzwa kwa bei ya juu Tsh500 wakati vocha hizo kiuhalali zinauzwa
kwa Tsh 450. Vocha hizi za Tsh450 zimetolewa katika soko ili
kuwawezesha wateja wetu kuwa na mawasiliano ya urahisi zaidi. Bei halali
ya vocha hii ni Tsh450 kama ilivyo andikwa kwenye
Vocha na tunawahimiza wateja wetu wanunue vocha hizo kwa bei
halali iliyotangazwa,siyo vinginevyo.
Tunashukuru kwa maoni yenu juu ya hili swala na
tunafatilia kwa ukaribu zaidi kwa wauzaji
wa vocha hizi kuhakikisha wanatoa huduma bora
na ya uhakika kwa wateja wetu na wananchi kwa ujumla.
Tafadhali shirikiana
nasi kwa kutoa taarifa mbalimbali hususani kuhusina na swala hili la vocha hizi za Tsh450 kupitia kurasa yetu ya
facebook na Twitter.
No comments:
Post a Comment