Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda asingoje kuzomewa tena
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
RAIS wangu, Waziri Mkuu, Mizengo
Kayanza Peter Pinda, amesikika akilia hadharani na kusema: “Kwa kweli hali ya
17-9-2012, ilinitisha sana. Kama mimi nimezomewa, kiongozi gani atakayesalimika
kuzomewa akienda uwanjani hapo?”
Aliyasema
hayo baada ya kuzomewa katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya
Sahara jijini Mwanza. Alipokuwa akiondoka msafara wake ulipopolewa kwa mawe!
Hili hakulisemea!
Hatuwezi
kukubali viongozi wetu wazomewe na kisha wafurumishwe kwa mawe kama vibaka.
Wanaosababisha haya kutokea wawe wananchi, au wawe viongozi wenyewe lazima
wadhibitiwe mara moja. Mashuhuda wanasema uwanja mzima ulizomea! Uwanja mzima
ulikuwa umelewa? Wanaoweza kulewesha uwanja mzima sasa basi, hawatufai!
No comments:
Post a Comment