Mzee John Malecela
Ndugu zangu waandishi wa habari, awali ya yote
naomba niwasalimie na niwapongeze kwa kufika -mwaka mpya 2014, pia naomba
niwapongeze kwa kazi kubwa ambayo mmekuwa mkiifanya hasa kuhakikisha watanzania
wanapata habari kwa kila jambo linaloendelea kila kona ya taifa letu la
Tanzania.
Ndugu waandishi wa habari nimewaita hapa ili
kuzungumza nanyi na mnisaidie kufikisha ujumbe kwa watanzania hasa kuhusu jambo
hili ambalo limekuwa gumzo kwa watanzania wengi la mbio za urais 2015 kwa
baadhi ya watu ndani ya chama changu cha mapinduzi (CCM), kilichonisukuma zaidi
na kupata hamu ya kuongea nanyi ni baada ya kumsikia -na kumuona kijana wetu
ndani ya chama cha mapinduzi bwana Paul Makonda akiwa na ujasiri wa kukemea
vitendo mambo haya yanayofanywa na baadhio ya viongozi bila uwoga wowote naomba
tuchukue fursa hii kumpongeza sana kijana huyu.
Nadiriki kusema nampongeza kijana huyu hasa kwa
kauli zake nzito na za kijasiri kwa maslahi ya chama changu cha CCM ili chama
kiendelee kupendwa na kuchaguliwa na watanzania.
Pia itakuwa si busara kama sitawapongeza vijana
wangu katibu mkuu wa chama ndugu ABDULRAHMAN KINANA na NAPE NNAUYE kwa juhudi
zao za dhati za kujenga chama na kuendelea kuwaeleza wananchi juu ya misingi
bora ya chama cha mapinduzi (CCM) kwa kuwakemea viongozi wasiofaa bila kujali
cheo na umaarufu wao ndani ya chama na serikali, nawaomba waendelee -na juhudi
zao hizo nami naziunga mkono juhudi zao na kama kuna watru wanaowabeza naomba
wasijali kwani kukemea viongozi wasiofaa ndani ya chama na serikali ni msingi
wa chama chochote kilichounda serikali.
Aidha nawaomba watanzania wenzangu wazalendo
wasikubali kukatishwa tama na kikundi cha watu wachache wasio na mapenzi mema
na taifa letu ambalo limekuwa mfano wa kuigwa kwa amani, upendo, utulivu na
mshikamano urithi tulioachiwa na baba yetu wa taifa mwalimu julias kambarage
nyerere ndani na nje ya mipaka ya bara letu la afrika.
Ndugu zangu waandishi wa habari naomba niwaambie
kuwa msemaji wa UVCCM kijana wetu Paul Makonda namuunga mkono kwa -kitendo
chake cha ujasiri cha kumkemea ndugu EDWARD NGOYAI LOWASSA bila uwoga kwa jinsi
anavyokivuruga chama chetu kwa lengo la kutaka urais 2015 huku secretariet ya
chama ikiwa imekaa kimya wakati inajua kuwa muda wa kuanza mbio hizi bado na
kufanya hivi kwa sasa ni kukiuka misingi na katiba -ya chama. Hapa najiuliza
kuwa ile misingi imara ya uongozi ndani ya chama chetu cha mapinduzi iko wapi?
Mpaka tumuachie mototo ndio akemee haya? Je, hapa chama kiko wapi?
Ukweli ni kwamba wanachama wetu na vijana wamekuwa
njia panda huku wakitamani kusikia tamko au karipio la chama juu ya suala hili
la harakati za urais 2015 bila mafanikio.
Naomba niseme kuwa bila kuwa na karipio au tamko
la chama, hawa wanaotumia pesa zao hadharani kwa lengo la kutafuta umaarufu na
ushawishi kwa vijana ili kupata madaraka wanaharibu misingi yetu bora ya
uongozi iliyowekwa na waasisi wetu ndani ya chama.
Kinachonisikitisha zaidi ni kuona juhudu za
uongozi wa sasa wa chama ngazi ya juu ikiwa ni pamoja na sekretarieti
inayoongozwa na katibu mkuu ABDULRAHMANI KINANA na katibu mwenezi NAPE NNAUYE
za kutetea chama hiki zinatiwa mchanga.
Ninaomba juhudi hizi zisibezwe na watu wenye nia
njema na chama. Ukweli ni kwamba vijana hawa wamekuwa na juhudi kubwa sana ya
kujenga na kuimarisha chama chetu -kwa wananchi kila pembe ya taifa letu kwa
kukemea na kueleza misingi ya uongozi bora. Swali: Je! Chama hakioni haya mpaka
vijana ndio waone?
Kwa hili ni lazima tubadilike ili kujenga chama
chetu na naishauri -secretariet ya chama lazima ichukue hatua mara moja, kijana
huyu paul makonda asingesema haya yote kama hana uhakika wa ushahidi wa wa haya
aliyoyasema na nampongeza sana.
Vijana na wanachama wengi wa CCM wamekuwa na hamu
kwa muda mrefu ya kutaka kujua msimamo wa chama chao bila mafanikio na ndio
sababu ya baadhi ya-wengine kupoteza mwelekeo.
Sisi tulikijenga chama hiki kwa taabu sana
hapakuwa hata mtu mmoja aliyediriki kutumia fedha zake kutaka madaraka.
Nidhamu, busara na uchungu wa rasilimali za taifa
hili kwa maslahi ya wananchi ndio vilituongoza kufuata misingi na maadili ya
uongozi ndani ya chama na serikali, ndio maana tunaumia sana kuona chama sasa
kinataka kutekwa na wenye fedha kwa uchu wa madaraka, mpaka tunashangaa na
kujiuliza hizi pesa wanatoa wapi? Na haya madaraka wanayotaka kwa kununua ni
kwa maslahi ya nani? Huku
watanzania wakiendelea kuwa maskini.
Mfano hivi karibuni
baadhi ya viongozi wa chama ngazi ya juu wamejibishana kwenye vyombo vya
habari,vitendo hivi havina tija kwa chama na wala havileti umoja na mshikamano
ambao umedumu ndani chama kwa muda mrefu.
Mwisho Ninaomba
sekretarieti ichukue hatua haraka kama alivyoomba kijana wetu makonda na kweli
kuchelewa kuchukua hatua jambo hili kumejionyesha wazi kwamba utaleta
kutokuelewana ndani ya chama kusiko kuwa na lazima.
JOHN SAMWELI MALECELA
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
No comments:
Post a Comment