Utata umezidi kuibuka katika Bunge
Maalumu la Katiba kutokana na kutopatikana kwa hati ya Muungano wa Tanganyika
na Zanzibar na ile ya Sheria ya Baraza la Mapinduzi ya kuridhia Mkataba wa
Muungano.
Utata huo, umebainika katika Kamati
kadhaa siku moja tangu wajumbe wa Bunge hilo waanze kujadili sura ya kwanza na
ya sita ya Rasimu ya Katiba, zinazohusu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na
muundo wake.
Juzi Kamati namba 2 ilimwalika, Spika
Mstaafu wa Bunge la Muungano, Pius Msekwa kutoa ufafanuzi kuhusu hati hizo,
lakini uhalali wa saini zake uliibua malumbano makali. Msekwa aliitwa kutokana
na kwamba ndiye aliyekuwa Katibu wa Bunge la Tanganyika wakati huo.
No comments:
Post a Comment