Mzungu huyo ambaye jina tunalihifadhi,
alidaiwa kufanya tukio hilo la kinyama Mei 26, mwaka huu na inadaiwa Aneth
alipomkatalia, alimtimua nyumbani hapo kwa kumtupia virago.
Chanzo makini kilidai kuwa, baada ya
kutupiwa virago bila kupewa mshahara wake sambamba na kipigo, Aneth aliripoti
tukio hilo katika Kituo Kidogo cha Polisi cha Tabata, Dar na muda mfupi polisi
walifika nyumbani hapo lakini Mzungu huyo hakutoka ndani, akakataa kuzungumza
chochote
Taarifa zilidai kuwa, baada ya polisi
kukutana na kizingiti hicho, walimpigia simu kiongozi wao ambaye aliwaamuru
warudi kituoni wajipange upya.
Akisimulia zaidi ishu hiyo, Aneth alisema
polisi walipoondoka eneo hilo, umati uliochukizwa na kitendo hicho ulikusanyika
nje ya nyumba ili kumdhibiti ‘mtasha’ huyo kwa lolote.
Kuna jirani mmoja alipiga simu tena kituo
cha polisi alipoona hali ya hewa imechafuka ndipo polisi wakafika kwa mara
nyingine na difenda na kufanikiwa kuingia ndani kwa kutumia geti kubwa,
walipofika walikuta milango imefungwa lakini ilisemekana aliruka ukuta na
kutimkia kusikojulikana.
Polisi waliniambia nimpigie simu
ajisalimishe lakini nilipompigia alisema hayupo na kama tunamhitaji tukutane
sehemu huku na yeye akiwa na polisi wake
kilisema chanzo.
Mmiliki wa nyumba hiyo anayeishi Kigamboni,
Mr. Cris alipoulizwa kuhusiana na ishu hiyo, alikiri kupokea malalamiko na
manyanyaso kutoka kwa Aneth.
Akisimulia zaidi maisha anayoishi na Mzungu
huyo, Aneth alisema:
Alikuwa akinitafutia sababu za kunitimua
kwani hivi karibuni kwa bahati mbaya nilipoteza ufunguo wa ndani, akanipiga
mateke na kunisababishia maumivu makali mwilini kiasi cha kushindwa kutembea.
Lakini lililoniuma zaidi ni hili la
kunilazimisha eti nifanye mapenzi na mbwa wake, amekuwa akifanya hivyo mara kwa
mara mimi nikaona siyo sawa na nilipokataa ndipo yakanikuta hayo.
Aneth aliripoti matukio hayo katika Kituo
Kidogo cha Polisi Tabata na kupewa fomu ya matibabu (PF-3) sambamba na
kufunguliwa jalada la kesi namba TBT/RB/3132/2014/ SHAMBULIO na jalada la
uchunguzi lenye namba TBT/IR/1829/2014/UCHUNGUZI.
GPL
GPL
No comments:
Post a Comment