Rais Jakaya Kikwete akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa; Rashid Othman.
Na Karoli Vinsent
Idara ya Usalama wa Taifa (Tanzania
Intelligence and Security Service = TISS) imeingia kwenye shutuma nzito
kutokana kitendo chake cha kushindwa kumthibiti, jambazi mwenye uraia wa Nigeria
ambaye amekuwa akifanya uhalifu huku, jambazi huyo akijinadi kwamba hakuna wa kumchukulia
hatua hapa nchini.
Jambazi, huyo,ambaye anajulikana kwa
jina Kingsley O.Ugiagble ambae amekuwa akifanya ujambazi ndani ya nchi pamoja
na kumiliki mtambo wa kutengeneza fedha za Kimarekani “Dola” pamoja na za
ndani vilevile kufanya wizi kwenye hudama za benki ATM.
Uchunguzi, uliofanywa na Mwandishi
wa http://fullhabari.blogspot.com huu umebaini Jambazi huyo mwenye Asili ya
Nigeria ambaye anakaa maeneo ya Mbezi jijini Dar es Salaam, kwenye nyumba
ambayo yenye thamani ya shilingui milioni 250. Jambazi huyo amekuwa akihusika
na mtandao wa kutenganeza fedha batili za Kimarekani yaani Dola.
Chanzo hicho cha habari kilizidi kusema
Kingsley amekuwa anahusika kuleta silaha ambazo zimekuwa zikitumika katika
vitendo vya ujambazi nchini Tanzania, huku mamlaka husika zikishindwa
kumchukulia hatua.
Kingsley ambae amekuwa akijinadi
kwamba hakuna wa kumchukulia hatua kutokana kujuana na Watendaji wakubwa ndani
ya Idara nyeti ya Usalama wa Taifa, hata hivyo chanzo hicho cha habari
kilimtaja jambazi huyo kuhusika kumiliki mitambo miwili ya kutengeneza fedha bandia
ambayo hutumika kutengeneza noti ya shs.10000.
Ana mtambo mwingine unatengeneza
Dola za Kimarekani ambazo sio rahisi kuzitambua.Taarifa hiyo inasema fedha hizo
zipo kwenye mzunguko wa fedha kwa maana zikipitishwa kwenye utambuzi mara moja
ni vigumu kuzitambua mpaka utakaporudia mara mbili ndipo mashine hiyo
utambuzi inagoma.
Uchunguzi wa mwandishi wa http://fullhabari.blogspot.com huu amebani mtambo huo wa kutengeneza fedha
hizo bandia unahifadhiwa katika nyumba moja maeneo ya Kunduchi jijini Dar es
Salaam na kuendelea na mpango wake wa kudurufu fedha hizo huku Idara za Usalama
wa Taifa (TISS) na zingine zinazohusika na usalama zikimwogopa jambazi huyo.
Kingsley, ambaye ameingia nchini
kutoka nchini Nigeria bila ya pasipoti, tena wala bila hata fedha yeyote ambapo
amekuwa akipata fedha nyingi kutokana na hujuma hiyo anayofanya ndani ya nchi
kutokana vitendo hivyo vya kijambazi.
Kwa mujibu wa yyanzo vya kuamika
zinasema jambazi Kingsley kabla ya kuja nchini aliwahi kufanya vitendo hivyo
vya ujambazi katika nchi za Ghana, Kenya pamoja na Nigeria, ambapo hivi sasa
amehamina nchini na kuendelea na vitendo hivyo.
Akilizungumzia hili, kigogo mmoja kutoka
ndani Idara ya Usalama na ulinzi wa Taifa ambaye hakuta jina lake liandikwe
mtandaoni kwa kusema yeye sio msemaji wa Idara hiyo alisema mtandao wa jambazi
huyo ambae ni raia wa Nigeria ni mkubwa sana.
“Sikufichi mwandishi, huyo jambazi huyo
mtandao wake ni mkubwa sana ndio maana hata sisi kumchukulia hatua tunasuasua
tu, kwa sababu mara ya kwanza alikamatwa na kufika hatua ya kumrudisha kwao
Nigeria lakini sisi walinzi wa Usalama kwa jjaa zetu tukazungukana nyuma tukamrejesha
tena” alisema mpashaji huyo wa taarifa.
Duru hizo zinasema: jeuri
anayoionyesha Kingsley, inatokana na kuwa na uwezo wa juu kifedha ndio maana
kushindwa kuchukuliwa hatua, kwani vyombo vya habari vimekuwa vikifichua
vitendo vyake huku mamlaka zikisuasua kumchukulia hatua.
No comments:
Post a Comment