Thursday, February 22, 2007

Kiswahili kinavyoshika kasi!!


Forest Whitaker kama Idd Amin kwenye "The Last King of Scotland"

Wakati Rais Kikwete na watu mbalimbali nchini wamekuwa wakikipigia debe kiswahili kipande chati duniani. Tayari matokeo yameanza kuonekana kwa baadhi ya viongozi duniani kuongea kiswahili walau neno moja moja

Kuna filamu ambayo imeingiza maneno ya Kiswahili na inafanya vizuri katika tuzo mbalimbali duniani inayokwenda kwa jina la "The Last King of Scotland"

Filamu hiyo inayozungumzia tabia alizokuwa nazo Idi Amini katika utawala wake iliyoigizwa na Forest Whitaker hivyo kupelekea lugha ambayo ilikuwa inatumiwa na waaigizaji kuwa kiswahili.

Bila shaka wa style hii Kiingereza kitapanuka zaidi...nasi hatuna budi kukikuza Kiswahili kokote tulipo. na tupatapo nafasi

Source: http://www.darhotwire.com/dar/Maisha/2007/02/22/30060.html

No comments: