Sunday, February 25, 2007

Muda wa kukutana na Rais Kikwete mjini Oslo umebadilika!


Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atakutana na Watanzania waishio Norway mjini Oslo.

Jumatano: Tarehe 28. Februari 2007

MAHALI: Grand Hotel, mtaa wa Karl Johan, Oslo. Karibu na Bunge la Norway (Stortinget)

Saa: Mlango utakuwa wazi saa 17.00 – 17.45 Central European Time. Jamaa wa usalama watakuwepo mlangoni kuandikisha majina na anwani kwa wote watakaoingia.

Baada ya hapo mlango utafungwa! Tukimsubiri Rais. Mkutano utaanza saa 18.00

Tafadhali toa taarifa hii kwa Mtanzania/Watanzania unayem/wafahamu aishie/waishio Norway.

Mnaombwa kuzingatia muda, kufika kwa wakati na kukaa kabla ya Mheshimiwa Rais kuingia. Kuhusu mavazi, itapendeza tukiwa rasmi kwa vazi la heshima.

Mkutano huu unawahusu Watanzania na familia zao, Watanzania wenye uraia wa nchi zingine na familia zao.


Wenu,

Semboja, Mwamedi Jumanne.
(Katibu),
Chama Cha Watanzania Oslo (CCW Oslo).

Baruapepe: tanzania@online.no
Baruapepe: tanzaniamail@yahoo.com
Simu ya CCW Oslo ya mkononi: +47 90 80 69 01
Simu ya Semboja (mkononi): +47 95 78 21 96
Simu ya makamu mwenyekiti, Hassan Nganz´o : + 47 47 26 21 81
Simu ya makamu mwenyekiti, Hassan Nganz´o : + 47 99 33 09 31

No comments: