Tuesday, April 03, 2007

Kiswaglish kwa chati na Wabunge


Uharibifu wa lugha yetu safi inayohitaji ufasaha wa kuitangaza ya Kiswahili, huanzia Bungeni na kisha huenea mitaani kwa Watanzania wengine.

Hayo yamedhihirika wazi tena wakati mwingine live katika luninga zetu za Bongo, kutokana na tabia yao ya kuchanganya lugha hii na kiingereza.

Ni katika vikao vya bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania utasikia Wabunge wakichangia, kukosoa au kufafanua kitu kwa mchanganyiko wa lugha hizi mbili (kiswahili na kimombo).

Mara nyingi utasikia.. ” Mh Waziri katika hotuba yake alijaribu kutuconvince, lakini maelezo yake juu ya ile project ya kuupgrade ile barabara ya kutoka Wilayani hadi kijijini hayakufanyiwa kazi’’

Pamoja na maelezo kuwa huo ni msisitizo wa jambo aka kukazia point, bado kiswahili kinafahamika na kinatosha kufanya haya yote.

Lawama sasa zinaelekezwa kwa Wabunge waliotarajiwa kuwa wasimamizi na watangazaji wa kiswahili fasaha ikitiliwa maanani kwamba kimeteuliwa karibuni kuwa lugha inayofaa kutumika Umoja wa Afrika.

Hadi mitaani lugha imekuwa ndiyo hiyo hiyo kwa maneno kama ’’haturuhusu short time, amenilima memo, jamaa hatamind na mengine mengi yanayofanana na haya.

Hivi sasa mbali ya kutoka na mkakati mpya wa kutibu kusambaa kwa gonjwa hili, kasumba ya Wabunge imetakiwa kubadilika ili kuokoa lugha yetu na virusi hivi.

Chanzo cha habari: http://www.darhotwire.com/dar/Habari/2007/04/02/31447.html

2 comments:

Anonymous said...

Jamaa aliyetuma picha ya kikatuni anaonyesha mwekaji kumbukumbu mzuri sanaa! Anaonyesha anafanya au amefanya kazi Maktaba Kuu ya Taifa.

pwagu.na.pwaguzi@oslo.onlin.no

Anonymous said...

Nilisahau ni:

pwagu.na.pwaguzi@oslo.online.no

Pwagu na Pwaguzi