Thursday, August 30, 2007

Oslo-Norway yasikitishwa na uamuzi wa Ethiopia kuwafukuza wanadiplomasia wake sita

Baada ya serikali ya Ethiopia kutangaza kuwafukuza wanadiplomasia sita wa Norway, waziri wa mambo ya nje wa Norway Bw. Jonas Gahr Stoere alisema ameshangazwa na kusikitishwa na tukio hilo.

Bw. Stoere alisema Norway imeiandikia barua rasmi Ethiopia kuitaka izingatie upya uamuzi huo. Bw. Stoere pia alisisitiza kuwa, hii haina maana kuwa uhusiano wa kibalozi kati ya Norway na Ethiopia umesimamishwa. Alisema Norway imefanya maandalizi ya kuwaondoa wanadiplomasia wake kwa wakati.

Jonas Gahr Støre, Norwegian Foreign Affairs Minister.

No comments: