Thursday, August 30, 2007

Mama Salma Kikwete achaguliwa kuwa mjumbe mkutano mkuu wa CCM Taifa


Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete akipongezwa na baadhi ya wanachama wa Chama Cha mapinduzi CCM Wilaya ya Lindi mjini baada ya kuibuka mshindi na kuchaguliwa kuwa mjumbe wa Mkutano mkuu wa CCM Taifa katika uchaguzi uliofanyika Mjini Lindi jana.

Katika uchaguzi huo uliofanyika katika ukumbi wa Kanisa Katoliki wa Andrea Kagwa, mjini Lindi, Mama Kikwete alipata kura 406 kati ya kura 458 alizopigiwa yeye na wanachama wengine 14 wa CCM Lindi mjini walioomba nafasi hiyo na kuufanya ushindi huo kuwa wa asilimia 92.



No comments: