Sunday, September 16, 2007

Kwa wapenzi wa Bongo Flava

AY na Mwana FA wanakuja na album lao la kukata na shoka walilolip jina la Habari ndio hiyo ambayo tayari imekamilika ikiwa na songi nane kama Asubuhi,Fungua Shampeni, Binamu, Ngoja ageuke, Unajuaje, Bounce, Kula kwa macho na Habari ndiyo hiyo uliobeba albamu” katika album lao pia wameshirikisha vichwa ama wasaniii moto kabisa kutoka africa wakiwemo Lady Jaydee, Q-Chiller, Jose Chameleone na Tallia..., wakilonga zaidi Mwana FA na AY wamesema lengo la mradi huu kujiongezea mafanikio au tuite kujikwamua kimaisha, lakini kubwa lililopo mbele yao ni kujulikana mbali zaidi ya Afrika Mashariki. Wameshafanya shoo kibao katika nchi mbalimbali lakini bado wanatamani kuwa kimataifa, ndoto ambayo baada ya miaka kadhaa huenda ikatimia kwasababu wanahasira ya kufika mbali katika game..


Habari hizi toka: http://haki-hakingowi.blogspot.com/
Picha na pwagu.na.pwaguzi@oslo.online.no


1 comment:

Anonymous said...

mambo vp?
mi natoka sweden lakini sasa hv nakaa oslo, norway. Mi na rafiki yangu tulikaa dar kwa muda mwaka nusu na sasa tunataka kwenda kuangalia bongo flava artist hapa oslo. najua alikiba amefika na we labda unajua artist mwengine atakuja january au february?

asante sana, na Christmas njema =)