Mambo ya Bongo sasa hivi kiboko; kuna mashopingi moli kama ya mtoni, Maubungo Plaza Mayfair Plaza na maplaza mengine mengi tuuu! Maapatimenti, mariili esteti broka, mabangaloo, na maskai skrepa! halafu mabarabara ya kimtoni na madaraja kama lile
Mademu siku hizi wanang'aaaa! Kuna maMiss kata, miss tarafa, miss wilaya, miss mkoa, miss Tanzania, mpaka miss yunivasi!
Mafasheni shoo, madizaina, na mamodozi! Maselebriti wa vipaji vya kitaaluma, kisanii
kimichezo, kisiasa, ua kwa majina ya ukoo. Kuna Matamasha, mabonanza, na makonseti hatari tupu!
Aisha Madinda wa Twanga Pepeta
Redio stesheni za kumwaga siyo kama wakati ule idhaa tatu tu; taifa, biashara na eksteno sevisi iliyokuwa inafunguliwa kwa masaa maalumu na kipindi kimoja tu cha salamu siku za Jumapili mchana! Na tivii chaneli kibao siyo kama wakati tivii Zanzibar minara michache mitaa ya Upanga na Ostabei tena usalama wa taifa wasiione, ukionekana mnara utakuwa umeenda kinyume na Azimio
Eee bwana na magari mengine hata ughaibuni hamna sijui mabaluni, maviieksi, Mamuso, mahama, mafoo whili draivu, maleksuzi, yaani wee acha tu!
Elimu nayo sasa imepanda kuna mainteneshino skuli kuanzia nasari mpaka hai skuli na yunivesti siyo UDSM na SUA tu kuna mayunivesti kibao sijui Nyegezi, Sijui Mikocheni, Makumira, Tumaini, na jingine la nguvu linaangushwa Dodoma unaambiwa hilo yunivesti sijui litakuwa linachukuwa wanafunzi ngapi sijui kwa inteki, yaani hilo yunivesti litakuwa kama Kembriji, Oksfodi, au Havadi! Eee bwana eee!
Siku hizi simu siyo big dili!
Unaambiwa nilikuwa Nanyumbu, Mtwara vijijini ndani ndani huko nikakikuta kibibi kizeeee utafikiri hakikuwahi kuwa kitoto kichanga! Unajua nini? Kilikuwa na kimobiteli cha Nokia hizi ndogo ndogo kinaongea na sijui na nani? Mwenyewe nilizimia! Enzi za TTCL ilikuwa uende kibanda cha simu tena ukikikuta nzima una bahati sivyo sumni yako inaliwa na simu haifanyi kazi. Ua ukitumia simu za nyumbani siyo laini kuingiliana au unaweza kujikuta unasikiliza simu tano kwa wakati mmoja! Siku hizi hela yako tu bazi, seliteli, voda, mobiteli lakini mimi naiona seliteli ndiyo kiboko lakini voda nao moto! Jamaa wa posta kweli walikuwa wanatuzingua barua unaituma Kibaha toka Dar inachukuwa mwezi! Siku hizi teksi meseji au ukiona namna gani vipi unanda intaneti unatuma imeli!
Usafiri siku hizi siyo sijui ATC, UDA, sijui KAMATA, nyooo! Siku hizi mtu unataka kwenda Mwanza unapaki begi lako unaenda eyapoti unachagua bomba gani udandie Prisisheni, Igo, eyaTanzania au bomba lolote tu! Mabasi siku hizi kuna malakshari yana maeyahostesi kama wa kwenye ndege! Mabasi yana vyoo, tivii, slipingi kochi yaani kama mtoni tu!
Mimi ughaibuni wala sikuzimii. Jamaa wanaenda ughaibuni nasikia wakifika huko wanabeba maboksi na kukosha vizee. Siulimuona nanihii, alipoondoka kwenda ughaibuni alikuwa na mimba hiyoo mashavu utafikiri anapuliza moto! Karudi mimba imekatika, kakondaa utafikiri Msudani ya Kusini miguu kama mikono ya mawani, yaani utamuonea huruma! Unajua Bongo michoro yako tu! Misheni kibao inategemeana na wewe mwenyewe jinsi unavyopanga kete
From TANZANET MAILING LIST: list@tanzanet.org
Subject: [tanzanet] Bongo Kama Ulaya!
No comments:
Post a Comment