Sunday, September 16, 2007

Miss Tanzania 2007 katika jaribio la nanihii.....

Mnyetishaji wetu aliongeza, mbunge huyo ameshawatajia hoteli mbalimbali visiwani Zanzibar, anazoweza kuzitumia kurusha roho na Richa, mara mkakati wake utakapokamilika. “Kila siku anatwambia akimpata Richa lazima aende kulala naye kwenye hoteli moja kali Zanzibar, anasema Dar es Salaam itamnyima uhuru wa kujinafasi anavyotaka.

“Hivi sasa ameshawapa ‘dili’ wanawake wawili wa Kariakoo ambao sasa hivi wanahaha kumtafuta Richa au ikiwezekana wapate hata namba yake ya simu, ili iwe rahisi kumpata,” alisema mnyetishaji huyo. Mtoa habari wetu aliongeza, mbunge huyo anataka kufanikisha azma yake ya kumnasa Richa kabla ya Fainali za 57 za Miss World, zitakazofanyika Sanya, China, Desemba mwaka huu. Alisema: “Anataka kumpata kabla ya hapo ili Richa atakapokwenda Miss World, waondoke pamoja, kwakweli dada yetu asipokuwa makini, anaweza kuingia mkenge.”


Gazeti hili, liliwasiliana kwa simu na mbunge anayedaiwa kumtega Miss Tanzania, Richa Adhia ambapo maongezi yalikuwa kama ifuatavyo;

Wikienda: Mheshimiwa mbunge unaongea na Gazeti la Ijumaa Wikienda.
Mbunge: Vema, niwasaidie nini?
Wikienda: Mheshimiwa, kuna madai kwamba umekula yamini kumpata kimapenzi Richa Adhia, ni kweli au siyo kweli?
Mbunge: Nikiwajibu ni kweli, itawasaidia nini?
Wikienda: Siyo suala la kutusaidia, sisi tunataka ukweli?
Mbunge: Huo ukweli utawasaidia nini?
Wikienda: Mheshimiwa, kwanini hutaki kujibu swali?
Mbunge: Sikiliza, haya ni mambo yangu binafsi na hampaswi kuyaingilia, (akakata simu).

Akiongea na mwandishi wetu, wiki iliyopita, jijini Dar es Salaam, Mratibu wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga alisema, Richa ni mtu mzima, kwahiyo uamuzi ni wake mwenyewe kumkubali au kumkataa mbunge huyo.

“Sisi tunawachagua warembo waliotimiza umri wa miaka 18, Richa ni mtu mzima, hatuwezi kumuingilia, uamuzi wa nani awe mpenzi wake ni juu yake mwenyewe,” alisema Lundenga. Hata hivyo, Lundenga alimsifu Richa kama mrembo mwenye nidhamu ambaye anamuamini hatolipa sifa mbaya Taji la Miss Tanzania. “Najua kuna vita kali ya kuichafua Miss Tanzania, lakini haitawezekana kwa kumtumia Richa, huyu atakuwa mfano bora kwa warembo wengine wote,” alisema Lundenga. Ijumaa Wikienda linamuasa Richa kuwa makini na mbunge huyo kwani hana nia njema, kwanza ni mume wa mtu na watoto. Siye huyo tu, watamfuata wengi kwa ‘gia’ tofauti, lakini muhimu ni kujichunga na kutambua dhima aliyonayo kama Miss Tanzania.

Kutoka gazeti la Ijumaa, Wikienda.


No comments: