Monday, October 29, 2007

Rais Mtahafu, Alhaj Ali Hassan Mwinyi

Alipoingia madarakani kumpokea aliyekuwa Raisi wa Awamu ya kwanza,Mwalimu Julius Nyerere mnamo tarehe 5 Novemba mwaka 1985, watanzania wachache sana (kama wapo) waliweza kutabiri kwamba miaka kumi baadaye na zaidi baada ya kustaafu rasmi, ataibuka kuwa mmojawapo wa maraisi wa Tanzania ambao watabakia kupendwa na kuheshimika kwa namna ya kipekee kabisa. Tunadiriki kusema “namna ya kipekee” kwa sababu ukweli unabakia kwamba inapofanyika tathmini ya uongozi wake, bado mtu au watu mbalimbali wanakuwa na maoni yao tofauti tofauti kuhusiana na suala hilo. Utoaji huo wa tathmini ni suala ambalo haliwezi kukoma leo wala kesho, ni tukio linaloendea na litakaloendelea, vizazi mpaka vizazi. Huo ndio uzuri au ubaya wa historia na muda (history and time),huwa vina jinsi ya kipekee katika kutoa hukumu zao.

Mpaka anakabidhi madaraka yake ya uraisi kwa raisi wa awamu ya tatu, Mheshimiwa Benjamin William Mkapa mnamo tarehe 23 November mwaka 1995, jina ambalo wengi tulipenda kulitumia ni “Mzee Rukhsa” ingawa kamwe hatukuwahi kusahau kwamba jina lake kamili ni Ali Hassan Mwinyi, Raisi wa awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania. (more…)

Kutoka: Bongo Celebrity.

No comments: