Monday, October 29, 2007

FAKE PASTORS

Baada ya kusubiriwa kwa muda mrefu hatimaye filamu ya Fake Pastors sasa inaingia mitaani. Kabla hata ya kutoka rasmi filamu hii tayari ilishakuwa gumzo mitaani kutokana na simulizi (hadithi) yenyewe ambayo kwa namna moja au nyingine imegubikwa katika jina la filamu yenyewe.Pichani juu ni cover ya filamu hiyo.

Kuanzia kesho jumatatu DVD’s na VHS’s za filamu hiyo zinapatikana madukani kote nchini Tanzania kwa bei ya Tshs 5,000(rejareja) na Tshs 3,500 kwa bei ya jumla.Filamu hii ni ya takribani masaa mawili na ina subtitles za kiingereza mahususi kabisa kwa wale wasiofahamu Kiswahili ambayo ndio lugha kuu iliyotumika. Wahi kuitazama na kisha utupe mapitio (review) yako.

Kutoka: Bongo Celebrity


No comments: