Wednesday, October 24, 2007





Balozi wa Marekani kujibu maswali moja kwa moja kupitia mtandao

na Mwandishi Wetu

BALOZI wa Marekani nchini, Mark Green, atajibu maswali kutoka kwa Watanzania kupitia mjadala wa moja kwa moja, kwa njia ya mtandao wa kompyuta, uliopangwa kufanyika Jumatatu ijayo kuanzia saa tisa alasiri.

Taarifa iliyotolewa na ubalozi huo jana ilieleza kuwa katika kipindi hicho cha maswali na majibu, Balozi Green atajadili kuhusu msaada wa dola milioni 698 ulioidhiniswa hivi karibuni, utakaosaidia kupunguza umaskini nchini.

Taarifa hiyo inamnukuu Balozi Green akisema kuwa huenda maneno ‘MCC’ na ‘Sheria ya Millennium Challenge’ yakawachanganya baadhi ya watu hapo mwanzoni, lakini baada ya muda kidogo, Watanzania watajifunza jinsi mpango huo unavyoweza kuleta tofauti kubwa kwatika maisha yao.

Ili uweze kujiandikisha kushiriki kwenye mjadala huu wa mtandao, tumia anuani yako ya baruapepe kuingia kwenye ukurasa wa tovuti ya webchat.state.gov.

Unaweza pia kuingia kwenye mjadala huo wa mtandao kupitia ukurasa wa tovuti ya ubalozi; tanzania.usembassy.gov.

Kutoka Tanzania Daima

No comments: