Saturday, October 27, 2007


KINGWENDU KINGWENDULILE


Ukiacha wachekeshaji (comedians) wanaounda kundi la Ze Comedy, wachekeshaji wengine ambao ni maarufu nchini Tanzania ni Kingwendu Kingwendulile (pichani). Bado hatuna uhakika kama jina “Kingwendu” ni jina lake halisi au ni la kisanii tu (mwenye uhakika tusaidie). Mojawapo ya misemo ya mitaani ambayo huyu bwana anapewa sifa ya “mwanzilishi” ni ule wa “hello hello” msemo ambao kimsingi ni kibwagizo tu cha mitaani chenye uwezo wa kuwa na maana lukuki. Siku hizi hasikiki sana kwenye anga za uchekeshaji na hivyo tunafanya juhudi za kujua yuko wapi na anafanya nini.

No comments: