washitakiwa
Mahakama ya Hakiumu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam jana iliwasomea mashtaka ya tuhuma za mauaji askari wawili wa usalama wa Taifa Abdulahman Omary (31) na Robert Nasting (23) pamoja na mtunza bustani wa Usalama wa Taifa Peter Saulo ambao wanatuhumiwa kumuua Siwengi Anthon....
Akiwasomea mashtaka hayo Mwendesha Mashtaka wa Polisi katika mahakama hiyo Boniface Edwin mbele ya hakimu Sundi Fimbo alidai kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaiwa kutenda kosa hilo mnamo Oktoba 3 mwaka huu majira ya saa nne asubuhi huko Mikocheni wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Mwendesha mashitaka huyo aliendelea kudai kuwa siku hiyo kwa pamoja watuhumiwa wanadaiwa kumuua Siwengi Anthon hali wakijua kuwa ni kinyume cha sheria.
Hata hivyo, watuhumiwa hao walikana mashtaka hayo na kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 6 Mwaka huu itakapotajwa tena na watuhumiwa walirudishwa rumande.
Kutoka: GlobalPublisherstz

No comments:
Post a Comment