Wananchi wa Kijiji cha Ukalawa wilayani ya Urambo wamemwambia RC wa Iringa, Amina Mrisho hawatatumia kondomu wakidai zinachangia maambukizo ya Ukimwi.
Walisema hakuna sababu i ya wananchi kuendelea kuhamasishwa kutumia kondomu zinazochochea maambukizi ya Ukimwi hususan katika kipindi kama hiki cha kampeni ya
kitaifa ya upimaji wa VVU.
Mrisho alikuwa kijijini hapo kukagua shughuli za maendeleo. Alipowauliza wanakijiji kama wanataka kuendelea kufanya ngono zembe, waliitikia kwa sauti kubwa kukubali kufanya hivyo.
Ofisa Afya wa Mkoa, Likaganga Likaganga alipojaribu kuwashawishi kutumia kondomu kwa madai kuwa baadhi yao wameshindwa kufuata amri kumi za Mungu ikiwapo ile ya sita
inayowakataza kuzini, pia hakuelewa somo.
Kwa mujibu wa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya Njombe, maambukizo ya Ukimwi wilayani hapo yamefikia asilimia 20 kutoka asilimia 12.3 za mwaka jana.
Katika hatua nyingine, Mkuu wa Mkoa hakuridhishwa na takwimu za watu 17,000 waliojitokeza kupima kutokana na idadi kuwa ndogo tofauti na watu 44,000 waliolengwa.
Kutoka: DarHotWire
No comments:
Post a Comment