Saturday, October 27, 2007

Ndo´ utamaduni wa kizazi kipya au!?
Catherine Kassaly na Mariam Mdeme.

Pati ya kuzaliwa Miss Mara mwaka 2002-2003 ambaye pia alishiriki katika kinyang´anyiro cha kumsaka Miss Tanzania, Rashida Wanjara iliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam, iligubikwa na mambo ya aibu (uchafu mtupu).

Pati hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa Much More uliopo katikati ya jiji Oktoba 19, mwaka huu na kuhudhuriwa na mastaa kadhaa wa kike na kiume ambapo baadhi yao walifanya mambo ya laana kiasi cha kuwafanya wastaraabu wachache waliokuwepo ukumbini kuinamisha nyuso zao kwa aibu......


Waandishi wetu waliokuwepo ukumbini hapo walishuhudia mastaa hao wakipata kilevi, kukumbatiana, kubusiana na kulishana vyakula kwa kutumia midomo bila wasiwasi na wengine kufikia hatua ya kupigana madenda laivu.

Aidha, mastaa wa kike walifunika kwa kuvaa vivazi vya ajabu vilivyoacha sehemu kubwa ya miili yao wazi na kupita navyo huku na huko ukumbini hapo bila kuona aibu.


Akiongea na Ijumaa Miss mmoja aliyeonekana kustaarabika ambaye ni mmoja wa waalikwa (jina linahifadhiwa) alisema kuwa, ingawa amewahi kuhudhuria pati kadhaa za mastaa wa hapa Bongo, ya Rashida ilikuwa imevunja rekodi kwa vituko vya aibu.

Sijawahi kuhudhuria pati iliyotawaliwa na uchafu kama hii, sawa kuna mambo ya kizungu lakini hii ni laana "this is too much", alisema Mrembo huyo aliyetokea kujizolea umaarufu katika siku za hivi karibuni.

Vituko vingine vilivyojiri katika pati hiyo ni pamoja na mwanamuziki wa kizazi kipya kutoka Kundi la Wanaume Family, Mh.Temba kumvamia msichana mmoja aliyekuwepo ukumbini hapo na kumpa kipigo kikali kwa kile alichodai kuwa ni kumfuata fuata katika maisha yake ya kimapenzi.

Hata hivyo, licha ya matukio hayo machache ya aibu yaliyojiri, sherehe hiyo ilifana vilivyo kwani watu walikunywa, wakala na kucheza katika kupomngeza mrembo huyo kutimiza miaka 24.

Baadhi ya mastaa waliohudhuria katika pati hiyo ni mtangazaji wa Kituo cha Televishen cha Channel 5, Ben Kinyaiya, Mtangazaji Adam Mchomvu wa Redio Clauds ya jijini Dar es Salaam, mwanamuziki Dully Sykes, mwanamitindo Fidelin Iranga, mrembo Nurgis Mohamed, Fania Hassan ambaye ni Miss Utalii na wengineo.

Kutoka Global Publishers TZ.

Soma makala:

Tumeacha watoto walelewe na televisheni (Tanzania daima)



No comments: