Thursday, October 25, 2007

Salome Mbatia. Picha kutoka: http://haki-hakingowi.blogspot.com/

Lori lilosababisha ajali na kupoteza maisha ya naibu waziri wa mandeleo ya jamii, jinsia na watoto Mh Salome mbatia likionekana katika eneo la ajali iliyotokeasehemu za kibena jana jioni na kusababisha vifo vya watu watatu hapo hapo akiwepodreva wa gari la mizigo aina ya Fuso na Dreva wa Mh Salome Mbatia. (Picha hii kwa hisani ya (MB) Zitto Kabwe)






Waziri Salome Mbatia afariki dunia

*Gari lake lagongana uso kwa uso na lori Fusso
*Waokoaji walazimika kukata mabati kuwatoa

Na Waandishi Wetu, Dar, Iringa

NAIBU Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Bibi Salome Mbatia, amefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea jana saa 10: 45 eneo la Kibena Factory wilayani Njombe
mkoani Iringa.

Akithibitisha kutokea kifo hicho kwa njia ya simu kutoka eneo la tukio, Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Dkt. David Mathayo, alisema marehemu Mbatia alikumbwa na mkasa huo akiwa safarini kutoka Dar es Salaam kuelekea Njombe, akiwa katika gari lake binafsi,

Nissan Patrol namba T 724 AGZ......(More)

No comments: