Wednesday, October 31, 2007

Waziri wa JK atekwa usiku...

Na Makongoro Oging.

Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Emmanuel John Nchimbi alitekwa na watu wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hali iliyomfanya apige simu polisi kuomba msaada kunasuliwa mkononi mwa wanachama hao.

Tukio hilo la kusikitisha lilitokea Ijumaa iliyopita majira ya saa 2.00 usiku mjini Songea mkoani Ruvuma saa chache baada ya kutoka katika kampeni ya udiwani, nafasi iliyoachwa wazi na marehemu Adam Mwaibabile katika Kata ya Majengo.

Vyanzo vyetu vya habari zilizopatikana hapa jijini Dar es salaam na huko Songea zinadai kuwa Mhe. Nchimbi mara baada ya kumaliza kampeni waliongozana na katibu, mwenyekiti wa wilaya hiyo na wanachama wa Chama cha Mapinduzi hadi nyumbani kwa katibu.....(Soma zaidi)

No comments: