Tuesday, October 30, 2007


Wazungu wakamatwa Chad wakitaka kutorosha watoto.

Serikali ya Chad imewakamata wazungu kumi na sita, wakiwemo raia tisa wa Kifaransa, waliotaka kutorosha watoto zaidi ya 100 kutoka Chad. Raia hao wa Kifaransa ni kutoka asasi isiyo ya kiserikali ijulikanayo kama Zoe´s Ark. Wafaransa hao tisa walidai kuwa walitaka kuwachukua watoto kutoka Darfur na kuwa ni watoto yatima. Huku serikali ya Chad ikidai kuwa watoto wao ni Wachad na siyo yatima kama wanavyodai raia hao wa Ufaranza.

Raia hao waliokamatwa wamedai kuwa serikali ya Ufaransa na ya Chad zinafahamu mpango wao huo na kuwa walipata idhini toka serikali zote mbili. Serikali ya Chad na ya Ufaransa zimekana madai ya raia hao.


Kwa habari zaidi soma:

http://edition.cnn.com/2007/WORLD/africa/10/30/
chad.france/index.html


http://news.bbc.co.uk/2/hi/africa/7069132.stm


Angalia kideo:

http://edition.cnn.com/2007/WORLD/africa/10/30/
chad.france/index.html#cnnSTCVideo

No comments: