Miss Tanzania namba tano mwaka 2007-08, Hadija Sula, ametoboa siri zake za mitego ya ngono dhidi ya ‘pedeshee’ marufu jijini Dar es Salaam ambaye amempandia dau hadi kutaka kumhonga gari na nyumba.Hadija alisema, amekuwa akifuatwa na ‘pedeshee’ huyo (jina tunalihifadhi), tangu Fainali za Miss Tanzania mwaka huu, zilipomalizika na kuongeza kwamba licha ya kumkatalia mara zote, lakini amekuwa akimganda kila siku.
Pedeshee aliyetajwa na Hadija ni mfanyabiashara maarufu ambaye ni mmoja kati ya ‘mapapaa’, wanaotajwa mara kwa mara kwenye nyimbo za bendi mbalimbali za Muziki wa Dansi nchini....
“Umiss kwangu ni tego la ukimwi, sasa sina raha ya kuishi, nyumba na gari vitanitokea puani,” alisema Hadija, wiki iliyopita jijini Dar es Salaam.Mrembo huyo aliongeza:
“Nimeshaambiwa kuwa jamaa ni muathirika wa ukimwi, yaani namuogopa kweli! Halafu hajaanzia kwangu, nasikia ni kawaida yake kuwalaghai mamiss kwa hizo pesa zake, lakini akishatimiza haja zake anaondoka.”
Alisema, mara ya kwanza kutokewa na pedeshee huyo, alimtumia mtangangazaji wa kike wa televisheni moja jijini (jina lake na kituo anachofanyia kazi, vinahifadhiwa) na kumuleza kwamba endapo angekubali kuwa nyumba ndogo yake, basi angeuaga umasikini.

Aliongeza kuwa sambamba na ujumbe huo, alioneshwa nyumba na gari ambalo angepewa mara baada ya kukubali ombi hilo:
“Nilishtuka, kwanza nilijiuliza iweje atumie gharama kubwa kunipata? Ninavyojua mimi mapenzi siyo pesa bali ni makubaliano.
“Si ajabu alikuwa ananifanyia danganya toto, siku moja angenigeuka na kuninyang’anya vyote, tumeona wangapi? Ukizingatia mimi mwenyewe namuogopa. Napenda kila mtu ajue mimi najiheshimu tena bado nasoma.”
Hadija ni mmoja kati ya warembo waliokuwa wakipewa nafasi kubwa ya kuibuka kidedea katika Fainali za Miss Tanzania mwaka huu, zilizompa taji Miss Kinondoni, Richa Adhia.Alipata nafasi ya kushiriki Miss Tanzania baada ya kufanya vizuri katika kinyang’anyiro cha kumsaka mlimbwende wa Kanda ya Ziwa ambapo aliibuka kinara. Uzuri wake wa sura na umbo, uwezo alionao katika kujieleza ndiyo pointi iliyomfanya ashingiliwe sana siku ya fainali.
No comments:
Post a Comment