Thursday, November 08, 2007




Rais Kikwete ateua Cisco, Biswaro mabalozi Malaysia, Brazil.



Abdul Omar Cisco Mtiro,
Balozi wetu mpya Malaysia.
Picha: http://haki-hakingowi.blogspot.com/


RAIS Jakaya Kikwete amewateua mabalozi wapya kuiwakilisha Tanzania katika nchi za Brazil na Malaysia.

Taarifa iliyotolewa jana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa imesema kuwa rais amemteua Balozi Joram Biswaro kuwa balozi wa Tanzania nchini Brazil na Balozi Abdul Cisco Mtiro kuwa balozi wa Tanzania nchini Malaysia. Uteuzi huo utaanza mara moja.

Kabla ya uteuzi huo, Balozi Biswaro alikuwa Mkurugenzi Idara ya Asia na Australia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Balozi Mtiro alikuwa Mkuu wa Itifaki katika wizara hiyo.

Pia Rais Kikwete amemteua Anthony Itatiro kuwa Balozi na Mkuu wa Idara ya Itifaki katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Itatiro alikuwa Mnikulu katika ofisi ya Rais.

1 comment:

Anonymous said...

cisco ametokea mbali. nilianza kumfahamu tokea alipokua angombea ubunge wa temeke na mrema. anastahili cheo hicho kwa utumishi wake mzuri kwa serikali.