Sunday, December 23, 2007

Haya mambo haya jamani!!! Ashakum si matusi


MKE WA DAKTARI AMWAGA

RAZI HADHARANI!


Maadili yanazidi kuporomoka kwenye jamii ya Kitanzania!!


Na Mwandishi wetu,Morogoro.

Mwanamke mmoja ambaye jina lake halikupatikana mara moja aliyetajwa kuwa ni mke wa daktari anayefanya kazi hospitali ya mkoa (jina lake linahifadhiwa), hivi karibuni alivua nguo hadharani ndani ya Ukumbi wa Mango Garden ulipo Nunge mkoani hapa.

Kwa mujibu wa mwandishi wetu aliyekuwemo ukumbini humo alisema mwanamke huyo alifanya tendo hilo la aibu Desemba 15, mwaka huu, wakati wa sherehe ya kumpongeza mtoto Jamila aliyetambuliwa na wazazi wake kama mtu aliyefikia utu uzima, maarufu kama kuvunja ungo......

Kinyume cha matarajio ya wazazi na waalikwa wa shughuli ya binti huyo iliyokusanya pia watoto wadogo, wake kwa waume, mke wa daktari alijikuta akigeuka kituko kwa kuvua nguo na kuziacha wazi sehemu zake nyeti, kisha kuonesha matendo ya aibu wakati akicheza wimbo wa Najiamini ulioimbwa na Kundi la Taarabu la Jahazi Morden.

Ilidaiwa kuwa kabla ya kufikia hatua hiyo, mwanamke huyo alikuwa ameshafanya vituko vingi vya kukera ambapo Muongozaji wa sherehe ‘MC’ aliwasihi wanaohusika wamtoe nje ya ukumbi ili kulinda heshima ya wanawake iliyokuwa ikivunjwa na ‘jimama’ huyo wa makamo.

“Kwanza alikuwa akicheza na chupa ya pombe na kuzunguka ukumbi mzima, kama mtu aliyepagawa na mapepo ndipo MC Nuru Choka aliposhauri atolewe nje lakini wahusika hawakufanya hivyo, kilichofuatia ni aibu,” alisema shuhuda wa tukio hilo.

Aliongeza kuwa licha ya kufanya tukio hilo, mwanamke huyo hakuonesha kujali ambapo alidiriki kuwaambia waliokuwa wakimkataza kuwa hakuna kitu cha kuficha katika dunia ya leo na hivyo kuomba aachwe amwage razi atakavyo.

“Ubaya uko wapi, anayeona aibu afunike macho yake, tusijiachie kwa nini?” alisikika akisema mama huyo aliyetajwa kuwa mmoja kati ya watu waliounda kamati ya kufanikisha sherehe hiyo.
Baadhi wa watu waliohudhuria shughuli hiyo, wakizungumza na mwandishi wetu walisema mwanamke huyo hakupaswa kusasambua mbele ya watu kwa madai kuwa hiyo haikuwa sherehe ya Kitchen Party ambayo wahusika huwa ni wanawake peke yao.


“Kimsingi kafanya jambo la aibu, ukizingatia mumewe ni mtu mwenye heshima sana, maana kama yeye hakuona tatizo alitakiwa amfikirie mumewe atajisikiaje akiambiwa vituko hivi?” alisema dada mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Asia.

Gazeti hili linalaani kitendo cha mwanamke huyo kuvua nguo hadharani na kuwaomba wanawake wengine wenye tabia kama hiyo waache mara moja ili kulinda maadili mema miongoni mwa Watanzania.

1 comment:

Anonymous said...

Wanaume wanafanya vitendo viovyu namna hiyo hiyo, na hakuna anayeandika maonyo juu yao. Wanauma kazi yao kuwarudi wanawake tu. Unafiki huu unatisha.