Ajira za Watoto wa Vigogo Benki
Kuu Zachunguzwa.
Kuu Zachunguzwa.
Na Mussa Juma, Arusha.
TAASISI za Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru) kwa kushirikiana na uongozi mpya wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), wameanza kuchunguza ajira za watoto wa vigogo wa serikali zaidi ya 17 ambao wameajiriwa katika benki hiyo ili kubaini kama ajira zao zilifuata taratibu.
Akizungumza na waandishi wa habari jana katika hoteli ya Impalla kabla ya kufungua mkutano wa 30 wa baraza la wafanyakazi wa benki hiyo,Gavana mpya wa benki kuu,Profesa Benno Ndulu alisema uchunguzi huo unafanywa kutokana na tuhuma ambazo zimewahi kuripotiwa na vyombo va habari.
Gavana Ndulu alisema ingawa sio makosa kwa watoto wa viongozi au ndugu kuajiriwa katika benki hiyo lakini wameamua kufanya uchunguzi huo ili kutazama kama kuna taratibu zilikiukwa au la na uchunguzi ukikamilika taarifa zitatolewa.
"Uchunguzi una miezi mitatu sasa na sisi tumekuwa tukioa ushashiriano unastahili kwa Takukuru tumewapa taarifa zote jinsi kazi zilivyotangazwa na alama walizopata katika usaili,"alisema Profesa Ndulu.
Alisema sambamba na uchunguzi huo wa ajira pia Takukuru kwa kushirikiana na managementi ya benki kuu wanazifanyia uchunguzi tuhuma zingine za ufisadi ambazo zilitolewa na Mbunge wa jimbo la Karatu Dk Wilbroad Slaa.
"Ni kweli kuna hizo tuhuma na zinachunguzwa na kazi hiyo ikikamilika pia taarifa zitatolewa,"alisema Gavana Mdalu.
Hata hivyo, alisema hivi sasa benki hiyo imejiwekea utaratibu wa kujichunguza wenyewe juu ya mfumo na usimamizi wa utekelezaji wa majukumu ya benki kuu.
"Tunataka kutenda kazi kwa uwazi kabisa bila kutegemea kufanyiwa uchunguzi na nia yetu ni kurejesha sifa ya benki kuu kwani tuhuma ambazo zimekuwa zikitolewa mara kwa mara dhidi ya benki kuu zinawakera,"alisema Gavana Ndulu.
Alisema hivi sasa wanakabiliwa na changamoto kadhaa zikiwamo kuboresha huduma za benki kuu,kuboresha ufanisi na utendaji na kusimamia utendaji wa mabenki hapa nchini.
Kuhusu hali ya uchumi alisema hivi sasa shilingi ya Tanzania imeanza kuimarika na akatoa wito kwa watanzania kujenga tabia ya kutumia fedha za hapa nchini katika matumizi mbalimbali badala ya dola za Marekani.
Alisema pia ucgunguz unaofanyika katika benki hiyo hivi sasa unahusu jengo ya jipya la twin tower na kwamba jengo hilo ni tofauti na majengo mengine lina vitu vingi ambavyo ni muhimu.
"Tunajiandaa hata nyie waandishi kuwatembeza katika majengo hayo mjionee na kuona vitu vilivyomo ndani kwani ni tofauti na majengo mengine,"alisema Profesa Ndulu.
"Tunajiandaa hata nyie waandishi kuwatembeza katika majengo hayo mjionee na kuona vitu vilivyomo ndani kwani ni tofauti na majengo mengine,"alisema Profesa Ndulu.
Baadaye akizungumza wakati anafungua mkutano wa baraza la wafanyakazi, aliwataka wafanyakazi kushirikiana na kuondoa mabaya yaliyopo katika benki hiyo.
Alisema jukumu lingine kubwa ni kujisafisha na kufanyakazi katika misingi ya uwazi ili kuhakikisha benki hiyo inarejesha heshma yake.
Awali, Gavana huyo alisema wanatarajia kuimarisha mahusiano na vyombo vya habari na kuanzia sasa kila baada ya miezi mitatu atakuwa akikutana na vyombo hivyo na pia kukutana na watendaji wa mabenki hapa nchini kila mwishoni mwa mwezi.
Kutoka: http://haki-hakingowi.blogspot.com/
Kutoka: http://haki-hakingowi.blogspot.com/
No comments:
Post a Comment