Saturday, January 12, 2008

Mapinduzi ya Zanzibar leo

Gongola hapa kusoma zaidi


Leo ni Siku ya Mapinduzi ya Zanzibar ambapo Watanzania wanaadhimisha siku ambayo wakazi wa visiwa vya Zanzibar waliung´oa utawala wa Kisultani miaka 43 iliyopita.

Katika kilele cha sherehe hizo ambazo zimekuwa zikiendelea kwa wiki nzima, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Amani Abeid Karume atawahutubia wananchi kutokea uwanja wa Amani, mjini Zanzibar.

Sherehe hizo zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali, akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mhe. Jakaya Kikwete na viongozi wa vyama vya siasa.

Sherehe hizo zilianza wiki nzima iliyopita kwa viongozi mbalimbali kushiriki katika miradi ya maendeleo na uwekaji wa mawe ya msingi ambapo Mhe. Karume alishiriki katika ujenzi wa nyumba za maendeleo za Michenzani na uzinduzi wa barabara ya Mpendae ambapo pia alipata fursa ya kuongea na wananchi na kueleza mikakati ya serikali kuwaletea maendeleo wananchi.

Aidha viongozi wengine walioshiriki katika sherehe hizo ni pamoja na Makamu wa Rais, Dakta Ali Mohamed Shein na Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mheshimiwa Shamsi Vuai Nahodha.



No comments: