
Kibaki sasa aomba msaada
kwa Kikwete
*Amtuma Uhuru Kenyatta
*Atua Dar na barua mkononi
*Odinga asema hawamwachi mkapa akimbie
*Wakenya wakabiliwa na kipindupindu
Ramadhan Semtawa, Taus Mbowe na Mashirika ya Habari
KATIKA kile kinachoonekana sasa ni kutafuta uungwaji mkono na nchi majirani, Rais Mwai Kibaki amemtuma mjumbe wake maalumu, Uhuru Kenyatta, kukutana na Rais Jakaya Kikwete kuzungumzia hali ya mambo yalivyo nchini humo.
Uamuzi huo wa Kibaki umekuja huku kukiwa na juhudi nyingine za kimataifa zinazofanyika nchini humo kwa ajili ya kuleta suluhu huku nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) isipokuwa Uganda, zikiwa kimya kuhusu upande gani zinaunga mkono. Hata hivyo, juhudi hizo zikiendelea jana Uhuru alikuwa Ikulu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufikisha ujumbe maalumu wa Rais Kibaki kwenda kwa Rais Kikwete. Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu, alithibitisha kuhusu ujio huo wa Uhuru na mazungumzo yake na Rais Kikwete Ikulu. Salva alifahamisha kwamba Uhuru alifika nchini akiwa ni mjumbe maalumu kutoka kwa Rais Kibaki ambaye pamoja na mambo mengine alimweleza Rais Kikwete hali halisi ya mambo yalivyo nchini Kenya. Alisema Uhuru alielezea kuhusu ghasia zinazoendelea nchini humo ili Tanzania ifahamu.
"Ni kweli Mheshimiwa Rais amekutana na ujumbe maalumu wa Rais Kibaki kutoka Kenya, alikuwa akipata briefing (muhtasari) wa mambo yalivyo nchini Kenya," alisema Salva.
Hata hivyo, alisema msimamo wa Tanzania kuhusu hali ilivyo nchini Kenya haujabadilika kwani bado unasisitiza umuhimu wa pande mbili kukaa pamoja katika meza ya mazungumzo.
"Mheshimiwa Rais amempokea na kufanya mazungumzo vizuri na mwakilishi huyo, lakini msimamo ni ulele kutaka pande zote zikae katika meza ya mazungumzo," alisema Salva.
Ujio wa Uhuru ambaye ni mtoto wa mwasisi wa taifa hilo, mzee Jomo Kenyatta, unaonekana kama hatua mpya ya Rais Kibaki kutafuta uungwaji mkono kutoka Tanzania kutokana na Uganda kutoa msimamo wa kumuunga mkono.
Tanzania hadi sasa haijatoa msimamo wa kuunga mkono upande wowote, badala yake imekuwa ikisisitiza umuhimu wa pande zote mbili kukaa katika meza moja ya mazungumzo.
Hali ya mambo nchini Kenya ilivurugika baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi wa Desemba 27, ambayo yamempa ushindi Rais Kibaki hivyo Chama cha ODM chini ya Raila Odinga kupinga na kutaka uchaguzi huo urudiwe chini ya serikali ya mpito ambayo itaitisha uchaguzi ndani ya kipindi cha miezi mitatu.
Kumekuwa na juhudi za kumaliza majeraha hayo ambazo ni pamoja na zile ambazo zilifanywa na Askofu Mkuu (mstaafu) wa Kanisa Anglikana nchini Afrika Kusini na Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel, Askofu Desmond Tutu na Waziri Mdogo wa Mambo ya Nje wa Marekani anayeshughulikia masuala ya Afrika, Jenday Frazer. Katika hatua nyingine, siku chache baada ya Rais Kibaki kusema yuko tayari kuunda serikali ya Umoja wa Kitaifa, mpinzani wake wa Raila alibeza kauli hiyo akisema kuwa kiongozi huyo hapaswi kutoa ahadi hiyo kwani hakushinda uchaguzi.
Odinga alisema hata kuteuliwa kwa mawaziri kutoka ODM katika serikali hiyo hakuwezi kuleta suluhu ya tatizo hilo na kusisitiza azma ya kuendelea na maandamano leo mpaka Kibaki ajiuzulu.
Akizungumza na waandishi wa habari jana,Odinga alisema ODM inaunga mkono juhudi za kimataifa za kuleta suluhu nchini humo lakini hakiwezi kukubali ahadi za mtu ambaye hakushinda. Odinga alisema chama chake kinahitaji suluhu ya kudumu ya tatizo hilo ambalo litapatikana kwa mazungumzo yenye kuzitangia mambo ya msingi.
"Kibaki hapaswi kutupa au kutueleza kitu chochote, kwa sababu anajua vizuri hakushinda uchaguzi," alisema Odinga.
Odinga alibeza pendekezo la Rais Kibaki akisema: "Huko ni kuwafanya watu Kenya wajinga, yani mtu aliyeshindwa anaita watu wengine kujiunga katika serikali ya mseto."
Alisema Kibaki amekuwa akiendelea kuongoza kutokana na idhini aliyopewa na wananchi katika uchaguzi wa mwaka 2002, ambayo alionya kuwa uongozi huo unakaribia kukoma hivi karibuni.
Hata hivyo, alisema anaweza kushiriki mazungumzo na Rais Kibaki chini ya usuluhishi wa Rais John Kufuor wa Ghana ambaye pia ni mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) ambaye alitua nchini humo juzi.****** "Kama Kibaki ni muumini wa kweli wa Katoliki, basi anapaswa kutamka hadharani kwamba hakushinda uchaguzi," alisema.
Hata hivyo, alisema anaweza kushiriki mazungumzo na Rais Kibaki chini ya usuluhishi wa Rais John Kufuor wa Ghana ambaye pia ni mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) ambaye alitua nchini humo juzi.****** "Kama Kibaki ni muumini wa kweli wa Katoliki, basi anapaswa kutamka hadharani kwamba hakushinda uchaguzi," alisema.
"Kutuchagua sisi katika baraza lake la mawaziri hakuwezi kutatua tatizo, hivyo hatuna haraka, serikali hiyo ni halali yetu," alisema Odinga na kuongeza:
"Tutaendelea na maandamano ya amani leo nchi nzima hadi Kibaki ajiuzulu," alisema Odinga. Mjini Nairobi, ODM bado inasisitiza kutaka kufanya mkutano katika uwanja wa Uhuru Park, ambako wamepigwa marufuku, huku maeneo mengine ya viwanja vya Babadogo, Kayole, Kawangware na Kamkunji, wakipanga kuendelea na maandamano hayo.
Alisema nchi hiyo inahitaji haki ya kweli na chombo imara cha kuleta suluhu kwa ajili ya kuziba makovu hayo na kuonya kwamba, bila haki hakuna amani. Katika hatua nyingine hali ya maisha nchini humo imeingia katika sura mpya baada ya mashirika ya kimataifa kuonya kuwa nchi hiyo inyemelewa na hatari ya kukumbwa na magonjwa ya mlipuko kikiwamo kipindupindu na kuhara kutokana na baadhi ya watu kulazimika kunywa maji yasiyo salama.
Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) lilisema juzi na jana, hali hiyo kukiwa na taarifa kuwa idadi ya watu wasiokuwa na makazi imeongezeka hadi kufikia 250,000 kutoka 180,0000. Shirika moja la misaada la Uingereza la Medical charity Merlin lilinukuriwa na BBC likisema kwamba mfumo wa usambazaji maji katika baadhi ya miji nchini Kenya sasa ni mibaya na hatari kwa afaya za binamu.
"Mfumo wa usambazaji maji katika baadhi ya miji ni hatari, hivyo kuna hofu ya kuzuka kwa magonjwa ya milipuko kama kuhara na kipindupindu," lilionya shirika hilo. Mkuregenzi wa shirika hilo nchini Kenya, Wubeshet Woldermariam alionya na kuomba suluhu ya kisiasa isipopatikana haraka kabla mambo kuharibika zaidi nchini humo. Alisema ni lazima kuwepo maridhiano ambayo yataondoa kitisho hicho ambacho kinaweza kuchochea ongezeko la mahitaji ya dawa za dharura.
"Kadri ghasia zinavyoendelea ndivyo pia hatari ya watu kukumbwa na matatizo ya kiafya inavyozidi kuwa kuwa kubwa," alionya.
Katika hatua nyingine, watu katika miji mbalimbali wamesali kwa ajili ya kuombea amani nchini humo.
"Viongozi wetu wametuangusha, wameleta matatizo katika nchi. Kwa hiyo tumeamua kuomba kwa Mungu ili aokoe Kenya yetu," alisema Jane Riungu, ambaye aliongoza watatoto wake watano kuelekea katika Kanisa la Hilltop nje kidogo ya Jiji la Nairobi. Wakati hali ikizidi kuwa ya wasiwasi huku pande mbili zinazopingana kila mmoja ukitoa mashariti yake, juhudi za kimataifa kuupatia ufumbuzi mgogoro huo zimezidi kuendelea.
Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) ambaye pia ni Rais Kufuorwa Ghana , anatarajia kuwasili nchini Kenya mapema wiki hii kukutana na pande zote zinazopingana ili kuhakikisha hali ya amani inapatikana nchini humo. Ujio wa Kuffor umetangauliwa na Askofu Mkuu mstaafu wa Kanisa Anglikana nchini Afrika Kusini, Desmond Tutu na Waziri Mdogo wa Mambo ya Nje wa Marekani anayeshughulikia Afrika, Jendayi Frazer.
Katika mazungumzo ya wapatanishi hao wawili, yalionyesha Kibaki kulegeza msimamo na kuonyesha utayari wa kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa huku Raila Odinga akipinga na kutaka ajiuzulu kisha iwepo serikali ya mpito itakaitisha uchaguzi ndani ya miezi mitatu. Hivyo, ujio wa mwenyekiti huyo wa AU unaonekenaka kama hatua nyingine zaidi za jumuiya ya kimataifa kuupatia suluhu mgogogoro huo ambao unatishia umwagaji damu mkubwa sawa na mauaji ya halaiki ya Rwanda ya mwaka 1994.
Wakati mataifa mbalimbali yakituma wawakilishi wake katika kuhakikisha hali ya nchi hiyo inarudi kama ilivyokuwa awali, Shirika la Msalaba Mwekundu (Red Cross), jana lilipeleka zaidi ya tani 7000 za vyakula mjini Mombasa ili kukabiliana na tatizo la njaa.
Kwa mujibu wa Shirika hilo chakula hicho kitaweza kusaidia zadi ya watu 30,000 wanaokabiliwa na uhaba wa chakula kwa kipindi cha mwenzi mmoja kutokana na hali katika mji huo kuwa mbaya. Kutokana na ghasia hizo, nchi ya Sudan nayo imekumbwa na uhaba mkubwa wa chakula kutokana na nchi hiyo kutegemea kwa kiasi kikubwa kuagiza chakula kutoka nchini Kenya.
Ukiacha Sudan, nchi nyingine zinazotegemea kuagiza bidhaa kutoka Kenya hasa mafuta zimekumbwa na uhaba mkubwa wa bidhaa hiyo hali inayotishia mustakabali kiuchumi.
Miongoni mwa nchi hizo ni Rwanda na Uganda, ambako kumekuwa na vipimo maalumu vya mafuta kwa watumiaji binafsi.
Ukiacha Sudan, nchi nyingine zinazotegemea kuagiza bidhaa kutoka Kenya hasa mafuta zimekumbwa na uhaba mkubwa wa bidhaa hiyo hali inayotishia mustakabali kiuchumi.
Miongoni mwa nchi hizo ni Rwanda na Uganda, ambako kumekuwa na vipimo maalumu vya mafuta kwa watumiaji binafsi.
Nchini Uganda, kuna ongezeko kubwa la bei kutoka Sh2400 za uuganda hadi Sh 5,000 kwa lita moja ya petroli. Wakati juhudi za kimataifa za kutafuta amani nchini Kenya zikishika kasi, ghasia na machafuko yamezidi kusambaa mjini Mombasa kufutia wafuasi wa ODM kuandamana kwa siku mbili mfululizo. Maandamano hayo yaliyoanza juzi nyakati za mchana mara baada ya sala ya Ijumaa yanahusiasha watu mbalimbali wakiwemo wanawake waliojiita 'wanawake wa Demokrasia wa Chungwa" pamoja na kikundi cha Mtandao wa Haki za Binadamu Pwani.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Reuters, waandamanaji hao walipita katikati ya barabara kubwa mjini hapo kwa lengo la kupeleka hati ya kufanya maandamano katika kituo cha polisi.
Waandamanaji hao walikuwa wakiongozwa na Mbunge wa ODM katika Jimbo la uchaguzi la Mvita lilolopo mjini Mombasa, Najib Balala pamoja na wabunge wa 12 wa chama hicho walitaka kuwasilisha hati ya kufanya mkutano leo katika kituo cha polisi cha Makupa kilichopo mjini Mombasa.
Waandamanaji hao walikuwa wakiongozwa na Mbunge wa ODM katika Jimbo la uchaguzi la Mvita lilolopo mjini Mombasa, Najib Balala pamoja na wabunge wa 12 wa chama hicho walitaka kuwasilisha hati ya kufanya mkutano leo katika kituo cha polisi cha Makupa kilichopo mjini Mombasa.
Polisi walilazimika kutumia mabomu ya kutoa machozi kwa lengo la kuwatawanya waandamanaji hao na kudhiditi maandamano hayo lakini waandamanaji hao waliwazidi nguvu polisi na kufika kituo hapo.
Inadaiwa viongozi hao wa ODM baada ya kufika kituoni hapo walitumia lugha kali kwa Mkuu wa Kituo (OCS) hicho, Leonard Baraza wakimtaka apokee hati hiyo ambapo alikataa na kumtaka kiongozi huyo aende peke yake bila wafuasia wake.
Sikiliza bwana OCS tumekuja hapa kukupa taarifa tu kuwa tutakuwa na mkutano siku ya Jumatatu (leo) na tunachotaka kutoka kwako ni ulinzi tu,?alisisitiza Balala na kuongeza kuwa wataendelea ratiba yao kama walivyopanga.
Barua hiyo waliyoicha juu ya meza ya Mkuu wa Kituo hicho. Baadhi ya maneno yaliyomo kwenye waraka hupo yanasema ?Taarifa ya maandamano ya amani Januari 7 (leo) katika mitaa ya Mombasa.
Awali, juzi Jeshi la Polisi lilifanikiwa kuzuia maandamano ya Waisilamu waliokuwa wakitoka katika ibada ya Ijumaa katika msikiti wa Sakina uliopo mjini Mombasa ambao walikuwa wakiongozwa na Balala kwa kuwatanya kutumia mabomu ya machozi na risasi za moto.
Mkuu wa Polisi wa Wilaya, Wilfred Mbithi, alionya wafuasi wa ODM na kusema kuwa maandamano hayo si halali na kwamba hayajaruhusiwa kisheria.
Mkuu wa Polisi wa Wilaya, Wilfred Mbithi, alionya wafuasi wa ODM na kusema kuwa maandamano hayo si halali na kwamba hayajaruhusiwa kisheria.
Vurugu za Kenya zimeingia jana zimeingia katika siku ya nane mfululizo kufuatia matokeo tata ya uchaguzi wa Desemba 27, mwaka jana yaliyomrejesha madrakani Rais Kibaki.
No comments:
Post a Comment