Mswahili asiyewahi
kufika Uswahilini:
Talib Kweli
kufika Uswahilini:
Talib Kweli

TALIB Kweli Greene ni moja ya nyota ya sanaa ya muziki nchini Marekani ambayo kwa muda mrefu sasa imekuwa iking’ara katika tasnia hiyo duniani. Greene ambaye alizaliwa Oktoba 3, mwaka 1975 katika kitongoji cha Brooklyn jijini New York nchini Marekani, kwa sasa anatambulika zaidi kwa mashabiki wake kwa jina la Talib Kweli.
Aina ya muziki anaoimba mkali huyo ni Hip hop Commercial ambao ni miongoni mwa mitindo inayokubalika zaidi na mashabiki wengi wa muziki duniani kwa sasa. Jina la msanii huyo ni mchanganyiko wa majina mawili ya Kiarabu na Kiswahili na katika mahojiano na jarida la Hip hop Stars la nchini Marekani hivi karibuni, alisema kwamba uswahili ndiyo asili yake na anajivunia kuwa mswahili japo hajawahi kufika uswahilini.
Talib ni jina la Kiarabu likimaanisha mwanafunzi na la pili yaani Kweli linatoka kwenye lugha ya Kiswahili, kwa maana hiyo anajiona kuwa ni mwanafunzi wa kweli kwakuwa katika maisha yake ni mtu wa kujifunza kila kukicha jambo ambalo anasema kuwa ndiyo maisha ya mwanadamu yeyote.
“Natambua kuwa mimi ni mweusi tena mswahili, hili ni jambo ninalojivunia nalo, lakini sijawahi kufika Afrika Mashariki kwenye asili ya Uswahili, japo ninaimani kuwa siku moja nitafika” alisema Kweli wakati wa mahojiano na Jarida la Hip hop Stars la Marekani, Septemba 2007.
Kweli ni Baba wa watoto wawili mmoja wa kiume na wa kike. Mtoto wake wa kwanza anajulikana kwa jina la Amani Fela na yule wa kike anaitwa Diani Eshe. Mkewe Talib Kweli

Licha ya ukweli kwamba Talib Kweli anapenda muziki lakini ni mmoja wa wasanii wa Marekani ambaye amekulia katika mazingira ya familia ya wasoni kwani wazazi wake wote ni maprofesa.
Mama yeke ni Profesa wa lugha ya Kiingereza wakati Baba yake ni Profesa wa masuala ya kijamii, lakini hilo halikuwa ni kikwazo kwake katika kuendeleza kipaji chake kwani alikuwa na marafiki wenye mwelekeo wa muziki kama De La Soul na wanachama wengine wa Kundi la Native Tongues Posse ambao walikutana wakati wakioma Sekondari.
Hali hiyo ya kupenda muziki iliendelea hadi Talib Kweli alipokuwa anasoma chuo kikuu cha New York (NYU) ambapo kipaji chake kiliendelea kuonekana japo wazazi walihitaji asome zaidi kabla ya kujiingiza katika fani.
Talib Kweli amefanya kazi na makampuni kadhaa ya muziki nchini Marekani tangu mwaka 1997. Makampuni hayo ni Rawkus Records, Blacksmith Records na Warner Bros Records ambayo tangu alipojiunga nayo mwaka 2005 anaendelea kudumu nayo hadi sasa.
Studio hiyo imeshafanya kazi za wasanii kadhaa kama vile, Just Blaze, DJ Quik, Kanye West na Jay-Z. Baadhi ya nyimbo ambazo zimemtambulisha Kweli katika gemu ni pamoja na Train of Thought, Get Em High, Get By, If skills sold na truth be told.
Nyingine ni I’d probably be, lyrically, Talib Kweli na Quality, ambayo ilikuwa ikisimulia watu makini katika jamii, huku akimzungumzia zaidi Rais wa kwanza Mwafrika nchini Afrika Kusini, Nelson Mandela.
Hivi karibuni wakati wa sherehe za kufunga mwaka 2007 na kuukaribisha 2008, Kweli akiwa na DJ Hi-Tek, alifanya ziara katika baadhi ya nchi za Ulaya, Amerika ya Kusini na Australia ili kuhakikisha kwamba anafanikiwa kujitangaza zaidi kimataifa.
Kweli anasema kwa sasa yupo mbioni kutoa albamu mpya iitwayo Prisoner of Conscious, ambayo anaamini itakuwa ni bora zaidi kushinda ya mwanamuziki yeyote nchini Marekani.
Makala haya yametayarishwa na Ahadi Kakore kwa msaada wa Jarida la Hip-hop Stars la nchini Marekani.
Kutoka Global Publishers TZ.
No comments:
Post a Comment