JESHI LA BUSH LAZUA
SONGOMBINGO DAR
Na Mwandishi Wetu
Ndege kubwa za Jeshi la Anga la Marekani, ambazo kwa wiki nzima sasa zinaonekana jijini Dar es Salaam, zimezua songombingo kubwa kwa wakazi wa jiji hilo ambao wengi walikumbwa na hofu kwa kudhani nchi imevamiwa....
Zikiwa katika umbo la kutisha, ndege hizo ambazo baadhi yake zimeegeshwa hadi katika eneo la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na kuonekana wazi na wengi, zilikuwa gumzo kubwa kutokana na jinsi zilivyo kubwa.
Baadhi ya wakazi wa eneo la Kitunda, ambako mara nyingi ndiko ndege zinazoingia katika uwanja huo zinaonekana kwa uwazi zaidi kutokana na kuwa eneo la chini zaidi kutoka usawa wa bahari, hivi karibuni walikimbia nyumba zao pale waliposhangaa kuona nyumba zao zinafunikwa na ndege hizo.
Huku wakiwa hawaamini kinachotokea, wakazi hao walidhani nchi imevamiwa na wengi walisahau hata watoto wao ndani ya nyumba.
“Hizi ndege ni balaa unajua wakati zinakuja hata mlio hatukusikia, tumeshangaa kuona kuna kivuli kikubwa kuangalia juu, tunaona ndege za ajabu ambazo zilituogofya sana.
“Mimi sikukumbuka hata kuchukua familia yangu, maana ilikuwa ni majira ya jioni na kwangu niliona kama nchi imevamiwa. Kusema kweli ndege hizi zinatisha mno,” alisema mkazi mmoja aliyejitambulisha kwa jina la John Mwita.
Mbali na hilo chanzo chetu cha kuaminika, kimetupasha kuwa tayari maafisa wa Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) na wale wa Kitengo cha Upelelezi (FBI), na kile cha United States Secret Service (kinahusika na ulinzi) wa Rais Bush, wapo nchini kwa wiki kadhaa sasa ili kuweka mambo sawa kabla ya ujio wa Rais George W. Bush atakayewasili nchini kesho.
“Hawa watu wako mtaani na wamejichimbia kweli, lakini Watanzania wengi hawajui kutokana na jinsi utendaji kazi wao ulivyo,” kilisema chanzo chetu.
Mbali na hilo chanzo chetu kilituhakikishia kuwa Jeshi la Marekani, ikiwa na maana ya Vikosi (United States Marine Corps) na (United States Navy) vya Majini na kile cha Anga (United States Air Force), tayari viko katika tahadhari kwa lolote litakalotokea na vimewasili nchini.
“Hapa nchini kikosi cha Marine cha Marekani kipo, lakini kimeongezewa nguvu zaidi kutoka katika base yao ya Djibout, ili lolote litakalotukia katika ziara yake kiweze kufanya kazi yake ipasavyo.
“Siyo hiyo tu kikosi hiki cha Marine kimeshatuma moja kati ya manowari zake, ili kuhakikisha usalama unakuwa mkubwa na wa kupitiliza zaidi.
“Kingine ambacho Watanzania wanapaswa kufahamu ni kuwa, simu zao zote zinafuatiliwa kwa karibu zaidi kuona nani anaongea nini na anaongea na nani na mazungumzo yepi. Hii wanadhibiti Wamarekani wenyewe moja kwa moja kutoka kwao.
“Teknolojia yao ipo juu, hivyo unapopigiwa au kupiga simu angalia sana katika kipindi hiki, maana usalama wa Rais Bush ndiyo agenda yao kuu ya kwanza,” kilisema chanzo chetu.
Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Marekani, Stephen Hadley juzi Jumatano, alizungumza na waandishi wa habari akiwa katika Ikulu ya Marekani na kuwafafanulia kwa kina kile ambacho Rais Bush anakuja kufanya nchini.
Hadley alisema, Rais Bush na mkewe Laura wataondoka rasmi Marekani leo hii kuja Afrika, ambapo watawasili Benin kesho na kukutana na Rais Yayi ambapo atakaa kwa muda mfupi kabla ya kupanda ndege na kuja Tanzania.
Keshokutwa Jumapili, Rais Bush atakutana na Rais Jakaya Kikwete na kusaini mkataba wa Millenium Challenge Corporation Compact kabla ya siku inayofuata kwenda Arusha ambapo atatembelea hospitali na Kiwanda cha A to Z na Februari 19, ataondoka nchini kuelekea Kigali, Rwanda.
Hadley alisisitiza kuwa anaamini ziara ya Bush nchini itakuwa ya mafanikio makubwa na kukuza ushirikiano kati ya nchi hizo na Bara la Afrika kwa ujumla.

Dege hili la aina ya B - 1 B Lancer Supersonic Bomber
ni moja ya madege yaliyotangulia Dar es Salaam
kufuatilia ziara ya Rais George W. Bush Jr.
nchini Tanzania itakayoanza kesho Jumamosi

Dege hili la aina ya Boeing B-52 Stratofortress is a long-range,
subsonic, jet-powered, strategic bomber ni moja ya madege
yaliyotangulia Dar es Salaam kufuatilia ziara ya Rais George W. Bush Jr.

No comments:
Post a Comment