Monday, February 18, 2008

Kipanya na ujio wa

Rais George W. Bush Jr.


Rais Bush akiwa

ziarani Arusha


Kiwanda cha A-Z cha vyandarua

Rais George Bush wa Marekani akimkubatia mmoja wa akina mama
waliowakabidhi vyandarua kwa ajili ya watoto wao wachanga kwa lengo la kujikinga na mbu wanaosababisha malaria,pamoja na mambo mengine Rais Bush leo ametoa tamko kuwa kwa kipindi cha miezi sita ijayo serikali ya Marekani ikishirikiana na benki ya dunia na Globa Fund watatoa mchango wa vitanda na neti million 5.2 bure kwa serikali ya Tanzania ikiwa ni utekelezaji wa ombi la Rais Jakaya Kikwete kwa Rais Bush, na hiii itasaidia kuepusha watoto kati ya mwaka mmoja na mitano kuugua ugonjwa wa malaria nchini Tanzania.


Rais George Bush wa marekani (wa pili kushoto) na mke Laura Bush wametembela kiwanda cha kutengeneza vyandarua cha A -Z Textile Mills kilichopo mkoani arusha muda mfupi baada ya kutoka hospitali ya Meru mkoani humo.


Rais George Bush wa Marekani (wa pili kushoto) na mke Laura Bush wametembela kiwanda cha kutengeneza vyandarua cha A -Z Textile Mills kilichopo mkoani Arusha muda mfupi baada ya kutoka hospitali ya Meru mkoani humo.



Hospitali ya Meru, Arusha.

Rais Geoge Bush wa marekani akiwa akiwa amemshika mama mjamzito baada ya kumkabidhi chandarua kwa ajili ya kujikinga na mbuu muda mfupi uliyopita alipotembelea hospitali ya wilaya ya Meru mkoani arusha, kushoto kwake
ni Dr Aziz Msuya wa hospitali hiyo.


Rais George W. Bush wa Marekani akishangaa akina mama wa Kimasai wakicheza ngoma ya kimasai muda mfupi uliyopita baada ya kutua Kilimanjaro International Airport in Arusha.Rais Bush amefwatana na mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete.


Rais wa Marekani George Bush akiwa na wagongwa kwenye hospitali ya wilaya ya Meru mkoani Arusha muda mfupi uliyopita.



Picha na habari kwa hisani ya:
http://haki-hakingowi.blogspot.com



Bush akitembelea shule


Bush akiwa na kinamama wa kimasai


Bush akipokewa Arusha


Aush akisalimiana na wafanyakazi wa hospitali ya Mount Meru


Bush na Laura wakiwa na baadhi ya wagonjwa waliofuata huduma hospitali ya Mount Meru





Bush akiwa na Wamasai


Bush akipiga stori na dk. Aziz Msuya wa hospitali ya wilaya ya Mount Meru
Picha kwa hisani ya: http://issamichuzi.blogspot.com



No comments: