Waziri wa familia, masuala ya watoto, na usawa, Manuela Ramin-Osmundsen amefukuzwa kazi ya uwaziri baada ya kumdanganya Waziri Mkuu, Jens Stoltenberg juu ya habari alizokuwa anaandamwa na na vyombo vya habari na wapinzani hapa Norway. Taarifa alizotoa Jens Stoltenberg ni kuwa Manuela alimwendea leo asubuhi na kumpa taarifa ambazo hapo mwanzoni hakuzitoa kwa Jens Stoltenberg alipomwomba atoe ukweli jana. Manuela alisema kuwa taarifa alizompa hadi jana ndizo zilikuwa za mwisho na za ukweli. Magazeti na vyombo vya habari zimetoa habari zaidi kuhusu uhusiano wa Manuela na wa Ida Hjort Kraby, dada mwanasheria ambaye majuzi tu alipewa kazi ya kuwa "ombudsman" wa watoto hapa Norway. Chanzo cha tatizo ni kuwa Manuela na Ida ni marafiki. Hapa Norway kupeana kazi kwa kujuana ni mwiko! Manuela alipoulizwa mara ya kwanza kama ana urafiki na Ida alikataa katakata. Vyombo vya habari vikawa vinachimbua na kuandika habari mpya za Manuela na Ida kila kukicha...
Habari zaidi angalia hizo zilizotangulia hapo chini.
http://watanzaniaoslo.blogspot.com/2008/02/
childrens-minister-under-fire-norways.html#links
No comments:
Post a Comment