Thursday, February 14, 2008


Ndege yaanguka, yaua

watu wawili Kilimanjaro


na Nakajumo James, Moshi


NDEGE ndogo imeanguka mjini Moshi na inahofiwa watu wawili, wamekufa na wengine, wawili, wakiwamo raia wa kigeni.

Ndege hiyo ilianguka jana mchana katika eneo la viwanda katika Manispaa ya Moshi, Kilimanjaro.

Mabaki ya ndege iliyoanguka jana


Meneja wa Uwanja Mdogo wa Moshi, MacDonald Kurwa, alisema waliokufa ni rubani Baraka Rutwaza (36) na Hyden Rowan (26), raia wa New Zealand.

Waliojeruhiwa ni Isaac Johannes (28) raia wa Afrika Kusini, na Sylan Borton, ambaye uraia wake haujajulikana. Majeruhi wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC mjini Moshi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Lucas Ng’hoboko, amethibitisha kuwapo kwa ajali hiyo jana, lakini alisema hajapata taarifa rasmi. Aliahidi kutoa taarifa kamili baadaye.

Watu walioshuhudia tukio hilo, wakiwamo Maua Salimu na Pasani Nyamba, walidai kwamba ajali ilitokea saa 8:40 mchana. Ndege hiyo ilikuwa na abiria watatu, na rubani.

Ndege iliyoanguka ni namba 5H-FUN, mali ya kampuni ya Serengeti Balloon Safari ya mjini Moshi.

Isaac alikuwa kiongozi wa kuruka angani, Haiden ambaye ni raia wa New Zealand na Regina ambaye hakutambuliwa uraia wake.

Ndege hiyo ilianguka eneo la mtaa wa viwanda na kuvunja uzio wa kituo cha mafuta katika barabara iendayo Kata ya Pasua na Mabogini mjini Moshi.

Akielezea tukio hilo, mmoja wa wafanyabiashara mjini hapa, ambaye hakutaka kutajwa jina lake, alisema ndege hiyo hutumiwa na watalii kwa ajili ya kuruka angani na parachuti.

“Kwa kawaida ndege huruka zaidi ya mita 10,000 usawa wa bahari…baadaye watu huruka na parachuti, lakini wakati rubani akitaka kupanda umbali huo alibaini kwamba kuna tatizo katika injini na kabla hajaamua lolote, ndege ikaanguka,” alidai.

Rubani inasemekana alijaribu kuwasiliana na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), lakini ilianguka kabla ya kupata msaada.Inadaiwa kwamba rubani wa ndege hiyo alifia eneo la tukio. Wengine walifariki dunia wakati wakipelekwa KCMC.

Askari wa kampuni ya ulinzi ya Ultimate Security walijaribu kuokoa, lakini hawakufanikiwa.

Vikosi vya zimamoto vya Manispaa ya Moshi vikiwa na magari SM 4648 na STK 4366, vilifika eneo la tukio.


2 comments:

Anonymous said...

any chance we can see this in english please

many thanks

Anonymous said...

was this cessna 5H-FUN short of fuel, was it overloaded, when can we see the AIB report ?

who owned it ?