Monday, February 18, 2008

Utiwaji wa saini jana Ikulu


Rais George Bush (kushoto) wa Marekani na Rais Jakaya Kikwete wakitia saini msaada wa Millenium Challenge Compact Agreement Ikulu jana jijini Dar es Salaaam ambapo Marekani imetoa msaada wa dola za kimarekani $700 million kwa ajili ya kupambana na umasikini, malaria, ukimwi na uboreshwaji miundombinu,msaada huu ni mkubwa kuliko yote iliyowahi kutolewa na serikali ya Marekani kwa nchi za Africa.

Rais Bush na Kikwete jana Ikulu..

Picha za juu ni Rais George Bush wa Marekani wakitia saini (jana) msaada mkubwa wa $ 700 Million kutoka serikali ya Marekani Marais George Bush mkataba huo umekusudia miradi mbalimbali ya maendeleo ukiwemo ujenzi wa barabara tatu ambazo ni barabara ya Tunduma hadi Sumbawanga,Tunduru Songea hadi Mbamba Bay na barabara ya Horohoro hadi Tanga na pia msaada huo mradi wa umeme katika mkoa wa Kigoma, mara baada ya kutia saini mlataba huo Rais Bush na Rais Kikwete walitembelea hospitali ya Amana iliyopo wilayani Ilala imepata mafanikio makubwa katika mradi wa mapambano dhidi ya Ukimwi ambap pia umedhaminiwa na serikali ya Marekani. Rais Bush anatarajia kwenda mkoani Arusha na kufanya shughuli ambako atalala na kurejea Dar es Salaam siku inayofuata na kuhitimisha Ziara yake nchini Tanzania na kuelekea Kigali nchini Rwanda.


Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam..

Rais Bush wa marekani akiwa na Rais Jakaya Kikwete walipotembelea hospitali ya Amana jijini Dar es salaam jioni.

Rice..

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Bi Condoleeza "Condi" Rice akiwasalimia wananchi alipokua anaingia Ikulu jijini Dar es Salaam jana.


Laura Bush..

Mke wa Rais, Salma Kikwete na Mke wa Rais wa Marekani, Laura Bush wakizindua The National Plan of Action, Pamoja Tutaweza,katika ofisi za WAMA jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii, Dk. Aisha Kigoda


Wageni..

Wageni mbalimbali walijitokeza leo kwenye viwanja vya ikulu jijini dar es salaam huku wakiwa wamevalia vitenge vyenye ujumbe wa karibu Rais Bus Tanzania kushuhudia utiwaji wa saini kati ya serikali ya Tanzania na marekani
ambapo serikali ya marekani imetoa msaada wa $700 million kwa Tanzania


picha na habari toka: http://haki-hakingowi.blogspot.com/



No comments: