Wednesday, March 12, 2008

CCM yajibu
KASHFA YA EPA


na Irene Mark


KASHFA ya ufisadi katika akaunti ya malipo ya madeni ya nje (EPA), imekishtua Chama Cha Mapinduzi (CCM), na sasa kinaamini kuwa suala hilo linatumiwa kisiasa kumdhoofisha Rais Jakaya Kikwete.

Taarifa iliyotolewa na kiongozi wa juu wa chama hicho inaeleza bayana kuwa CCM inaamini kwamba wanasiasa wa kambi ya upinzani, wanaitumia kashfa hiyo kwa malengo ya kupotosha ukweli na kuonya kuwa huo ni mchezo mchafu.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Kapteni John Chiligati, ameonya katika taarifa aliyoitoa jana jijini Dar es Salaam kuwa wanasiasa wanaotumia kashfa ya EPA kwa kukosoa utendaji wa Rais Kikwete, hawapaswi kuwapotosha wananchi kuhusiana na jinsi kiongozi huyo mkuu wa nchi alivyolishughulikia suala hilo.

“Katika hali hii, CCM tunayo kila sababu ya kuamini kwamba kashfa ya EPA imeanza kutumiwa kwa malengo ya kisiasa, ya kudhoofisha kazi nzuri inayofanywa na rais katika kushughulikia ufisadi na mafisadi… na kumdhoofisha rais aonekane hajafanya jambo lolote la maana. Njama hizi siyo za kiungwana na ni mchezo mchafu,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo na kuwataka wananchi wavute subira wakati timu inayochunguza tuhuma hizo ikiendelea na kazi yake.

Taarifa ya chama hicho imekuja siku mbili baada ya kauli iliyotolewa na Mwenyekiti wa taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe ikimhusisha Rais Kikwete na kuwalinda watuhumiwa wa kashfa ya EPA.

Katika kauli yake, Mbowe alisema mamlaka aliyonayo, yanampa nguvu Rais Kikwete kuwachukulia hatua za kisheria watuhumiwa wa ufisadi huo, lakini ameamua kukaa kimya na Mbowe alitafsiri ukimya huo kuwa sehemu ya ufisadi.

Hata hivyo, akitetea hatua zilizochukuliwa na Rais Kikwete, Chiligati alisema kuwa rais amefanya mambo makubwa kuhusiana na kashfa hiyo.

Akiyaorodhesha baadhi ya mambo hayo, Chiligati alibainisha kuwa Rais Kikwete ndiye aliyeamuru kazi ya ukaguzi wa EPA ifanywe na wataalamu kutoka nje, ambao ni Kampuni ya Ernst & Young na kuitangaza hadharani sehemu ya ripoti ya uchunguzi.

Aidha, pamoja na kutangaza hadharani, rais alichukua hatua kadhaa, ikiwamo ya kuunda timu ya viongozi wa serikali, chini ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kuchunguza kwa undani suala hilo na kuhakikisha kuwa fedha zilizoibwa zinarejeshwa na waliohusika wanachukuliwa hatua.

Ilieleza kwamba, lawama anazobebeshwa rais za kushindwa kuwapeleka mahakamani watuhumiwa wanaorudisha fedha hizo hazistahili kutolewa hivi sasa.

“Lawama hizi si sahihi, si wakati wake na zina lengo la kutimiza malengo ya kisiasa ya kulipaka matope jina la Rais Kikwete machoni mwa umma… hali hii haiwezi kukubalika machoni mwa jamii ya waungwana kama Watanzania tulivyo.

“Ni lazima wananchi wakatae njama na hila hizi zinazoendeshwa na baadhi ya wanasiasa wa vyama vya upinzani,” alisisitiza Chiligati.

Aidha, CCM imeshauri kuwepo kwa utamaduni wa kukosoana kwa lugha ya staha na uungwana badala ya dharau, kejeli na maudhi huku wakitolea mfano neno ‘uhuni’ alilodai lilitumiwa na Mbowe kwamba si la kistaarabu kutumiwa na mwanasiasa dhidi ya rais.

Chiligati aliwahakikishia wananchi kwamba baada ya kukamilika kwa uchunguzi wa timu iliyoundwa na Rais Kikwete, taarifa itatolewa na hatua stahili zitachukuliwa dhidi ya watuhumiwa wote.


juu

Maoni ya Wasomaji


Maoni 49 yameshatolewa. (Nawe toa maoni yako!)

Pamoja na uchungu ambao CCM inaweza ikawa nao kwa kauli dhidi ya Rais, ni muhimu wakaelewa kwamba wananchi wamechoka na "business as usual". Wanaomsema Mheshimiwa Rais sio kwamba wanamchukia kama amabvyo CCM ingetaka ieleweke, ni kwamba wamechoshwa na mambo yasiyoridhisha yanayotoka upande wa serikali.

Haiingii akilini kwamba kila mtu anaona ukweli isipokuwa watu wa serikali!! Hivi CCM wanataka kusema kwamba Rais hajui kwamba Mwanyika na Hosea ni watuhumiwa? Sasa ni sifa gani inayowaweka kwenye Kamati hii?

Vilevile, akina Chiligati inabidi waelewe kwamba nchi hii sio ya CCM peke yao, ni ya wananchi wote. Hii maana yake ni kwamba ni lazima waruhusu watu wenye mitazamo nje ya ule wa CCM watoe dukuduku zao. Wasiwawekee mipaka. Hapa tunapigania utaifa sio uanachama!! Wakati wa kulindana kichama umekwisha.

Rais afanye kinachotegemewa na wancnhi na atakuwa na raha mustarehe. Sasa hivi anaonekana kupwaya katika maamuzi yake, na inawezekana ni kwa sababu ya ushauri mbovu toka kwa watu wanaomzunguka, kama hawa waheshimiwa.

na Amk, Dar, - 12.03.08 @ 10:28 | #1735

Ndiyo, tumechoka na BUSINESS AS USUAL.Chiligatiatueleze wapi aliwahi kusikia mwizi anaambiwa arudishe kitu alichoiiba bila kufuata sheria. Serikali si mali ya chama wala mtu binafsi. Obama is clear on such issues, "We are tired with BUSINESS AS USUAL IN THE STATE HOUSE"

na Quara, Mwanza, - 12.03.08 @ 10:40 | #1739

Napenda kuchangia ka uchache katika mjadala huu wa EPA na shutuma za rais kutochukua hatua madhubuti.

Awali ya yote, ningependa kuunga mkono hoja kuwa si sahihi kumkejeli rais wa nchi kwa namna yoyote ile iwe kwa maneno au matendo.

kwanza kwa sababu sio uungwana a kitanzania wala wa kiafrika kumsema mkubwa kwa maneno ya dharau. Utamaduni wetu unatutaka kumsema kwa staha lakini anayesemwa kwa vile ni mtu mzima na busara zake atakuelewa na kujirekebisha.

Tusikimbilie sana ustaarabu wa watu wengine wanamazoea yao. na kwa kutumia maneno ya busara sio kuonyesha unyonge ni kuonyesha busara ulizonazo.

Ama suala la wajumbe wa tume, hebu tuwape muda pamoja na tuhuma zinazowakabili miezi sita sio mingi, tutatambua pumba na mchele.

haraka ya kuwataja na kuwapeleka mahakamani haitatusaidia. tuwaache wakusanye ushahidi ukikamilika watatutajia na kuwapeleka au kutowapeleka mahakamani. Kuna suala hata la nguvu za rais katika mabo ya kitaifa Tusubiri tusiharakishe tutakuta mwana si wetu.

mwisho

na bujaga izengo kadago, saut-mwanza, - 12.03.08 @ 10:45 | #1741

Sisi tunachotaka Rais wetu atende ni mwizi kukamatwa na kutangazwa hadharani. Hii itasaidia sana kuona kuwa sheria ni msumeno ukatao pande zote (Vigogo na kwa walalahoi). Bla bla hatutaki hata kidogo na tumechoka na talk shop tunachotaka vitendo kama tumshughurikiapo mwizi katika mitaa yetu.
Hebu jiulizeni, fedha hii ingeweza kusaidia wananchi wangapi walio na matatizo? Sioni sababu ya kucheka hapa!Maji yamemwagika waliohusika watendewe kile walichokitenda bila kuangalia sura zao, madaraka yao, urafiki wetu na wao kwa kuwa wameshaoza.
Sitaamini kuona suala kama hili linakuwa porojo tu na Balali eti hawajui na wala hawataki kusema aliondokaje nchini, anaumwa nini na kwa nini asiletwe mbele ya sheria ataje wahusika?

na Dominick, Mwanza, - 12.03.08 @ 10:55 | #1745

CCM ni chama cha majizi,mafisadi na walanguzi wa nchi hii,mi nasema ipo siku lazima tuuane nchi hii ndo ushenzi utaisha,anakataa nini JK kuitwa muhuni wakati ni kweli anaendesha nchi kisanii,Mwanyika atasema nini juu ya BOT wakati na yeye ni fisadi?what about ze boss of PCCB?!!!green deep company imo kenye kashfa na ndo ilinunua magari ya wilaya na mkoa ya CCM,yameandikwa Hundra,kwani hatujui?minasema hata Uingereza once time ilikuwa baba wa dunia,ikiwa na makoloni kila kona ya dunia hii,na kwa kiburi cha ubinadamu wao wakatoa na methali isemayo,!"The sun never set in England"Go East to the sun rise and find our colonies and go far west of the wolrd you will find our colonies too!!lakini leo Marekani ndo mbabe na wao ni waskilizaji tu wa mambo ya white house!nani alijua dola ya Rumi iliyokuwa na kiburi cha nidhamu ya jeshi na utwala wa dunia itaanguka?kibuli kilichowafanya wamtese mwana wa Mungu YESU KRISTO kisa anatishia usalama wa dola yao!!wko wapi leo ktk ulimwengu wa dunia!?wale waliofanya J'pili iwe mapumziko kwa dunia nzima,walioingizalugha ya kilatini kama lugha ya dunia ktk sayansi?hawapo tena na mwisho wao ni mbaya!ama hakika nabii shabani Robert alisema.uwingi wa busara haupimwi kwa uwingi wa mvi kichwani,bali hekima,malezi na matumizi mazuri ya elimu dunia,"viliba zee haviwezi kutunza ladha ya utamu wa mvinyo"...."let's say age is nothing than numbers"!!they have 31 years in numbers but five years in experience of people's ploblems!!the day will come when the yellow and green wilii turn to tears and blood

na mdanganyika, Tz, - 12.03.08 @ 10:56 | #1746

Unaweza kuielewa tabia ya mtu kutokana na rafiki zake wanaomzunguka.
kama Kikwete amezungukwa na Lowassa na Rostam ambao ni MAFISADI waandamizi kabla na baada ya kuingia kwenye uongozi Unategemea nini toka kwa Kikwete!!!!,definetely nae na fisadi tena mzuri tu. Kwa vile ameshika vyombo vyote vya dola na vyombo vyote ni corrupt tukubali tu matokeo amalize ngwe yake na aombe sana Mungu asijepatikana president mwenye roho ya uendawazimu Kikwete akiwa bado hai.Lazima amburuze mahakamani na kama hataki hili limtokee aache mambo ya kiswahili ya kuoneana haya,aanze kwa kuwaadabisha wadau wake wakuu Rostam na Lowasa then tuone mtanzania gani mwenye akili timamu atakaye msema ovyo president.

na Suleiman, Dsm, - 12.03.08 @ 11:05 | #1750

Hivi jamani nyinyi tuliowachagua mtuongoze mnafanya nini mbona mambo yanazidi kuwa mabaya na mnajifanya hamuoni ,mnaona tu pale ambapo Kikwete anapotajwa.Je hamna uchungu na nchi hii yaani hamjali .Sasa tuwaiteje,unajua inashangaza Viongozi wa juu wanaposhindwa kuona tatizo sasa hivi mnataka kutuyeyusha kuhusu report ya EPA nk.Enyi viongozi wa upinzani endeleeni kuwaamsha hawa maana bado wapo kwenye usingizi wa chama.

na queen, dsm, - 12.03.08 @ 11:20 | #1756

Mbowe hajakosea hata!
Raisi wetu kayataka mwenyewe hayo, kuendekeza uswahiba kwa majambazi na mafisadi ina muunganisha moja kwa moja naye kuonekana ni fisadi na jambazi kama wao!

kama hataki kuwa kundi lao ajitenge nao na aache sheria ichukue mkondo wake! Iweje yeye awe juu ya sheria na kuamua kipi kifanyike na kipi kisifanyike juu ya watuhumiwa?? aiache sheria iende kama ilivo.., suspect yaani watuhumiwa wote waswekwe ndani ili waisaidie vyema polisi na huo uchunguzi wa kisanii kwani sioni haja ya uchunguzi tena wakati ernest&young walisha anika kila kitu!

Tumechoka na usanii wako JK. ama unadhani watz wote hamnazo?? ni machungu na hasira ya kuona wezi wetu wanaendelea kupeta mitaani kwa baraka zako badala wawe nyumbani kwo segerea na keko!

na nyesi, Kanada, - 12.03.08 @ 11:29 | #1758

ukweli ni kwamba wengi wa wahusika wa kashfa ya EPA ni viongozi wa serikali au watu walio karibu na viongozi wa serikali.so kuwataja ni kama kuichafua serikali na kupoteza kabisa imani na serikali ya CCM.,JE,kama kamati teule ya bunge ilimtaja Lowasa KaramagI na Msabaha walitajwa kuhusika moja kwa moj au vinginevyo why hawa wezi ninao amini walishiriki katika kumuweka kikwete madarakani kwa kuchangia fedha za kampeni wasitajwe? Kikwete atakua anawalinda watu hawa .ITS NOT A SHAME TO HIM ONLY BUT A SHAME TO ALL THE CCM STAKE HOLDERS.huu ni mchezo mchafu na wa kuigiza kwani watanzania wanaoiba kuku,simu za mikononi wanachomwa moto mpaka kufakwanini hawa waliotusababishia umaskini wasishtakiwe angalao as a prize of what they call it sheria.but All in All OUR PRESIDENT IS not serious at all.ni msanii tu .that is why baba wa taifa aliyekua akimfahamu fika upeo wake wa kuelewa mambo alimkataa pamoja na rafiki yake wa karibu FISADI LOWASA NA KARAMAGI.

na alphonce, Dar es salaam, - 12.03.08 @ 11:35 | #1759

Tumechoka na usanii wa CCM. Watu wote tunajua Mwanyika na Hosea hawaqualify kua ktka hiyo kamati ya Rais ikiwa na maana JK anafanya usanii wa wazi ktk kutatua hili jambo.
Nashangaa mpaka leo Chiligati hajaona constructive side of opposition na kwamba toka tupate uhuru hadi leo CCM imeshindwa kudeliver.

na David, dsm, - 12.03.08 @ 11:36 | #1760

Naanza kuamini tetesi kwamba fedha za EPA zilitumika kufadhili kampeni za CCM 2005 na yale makampuni ni kanyaboya tu, na hata hela tunazoambiwa zimerudi ni uwongo ila wanatafuta njia ya kulindana hawa CCM. Iweje hela irudishwe halafu useme humjui aliyerudisha kama sio uwehu ni nini? ukienda msajili wa makampuni utakuta jina la kampuni na wamiliki wake, sasa iweje useme tumepata jina la kampuni tu la mhusika bado. Tafadhali tumechoka kufanywa wajinga, Bob Marley alisema, you can fool some people sometimes but you can't fool all the people all the time, hivyo tumeamka na tunadai haki zetu na msipotupa tutachukua wenyewe kwa kutumia nguvu ya wananchi kama walivyofanya Romania na Ukraine.

na j4, Dar, - 12.03.08 @ 11:36 | #1761

Napenda kuishauri CCM na Chiligati wake wajue kuwa suala la EPA siyo la CCM bali ni suala la kitaifa. Ndiyo maana taarifa ya Mheshimiwa Mbowe ilimsema "Rais" na siyo "Mwenyekiti wa CCM". Hapa tena acheni tuongelee masuala ya kitaifa kama walio na uchungu wa nchi hii inayotafunwa usiku na mchana kama vile haina wenyewe.

Mimi naona kusema kuna watu ambao wamerudisha fedha za EPA bila kutaka kuwataja majina yao na kiasi walichorudisha ni kiini macho tu. Suala mwizi yeyote akamatwe na apelekwe mahakamani na huko ndiko itakapodhihirika nani ana haki. Ni kigugumizi gani kinawapata kuwashitaki waliochomoa fedha nyingi hivyo ikiwa kibaka tu anayechomoa shilingi elfu moja au kuiba mkungu wa ndizi kijijini kwetu anapelekwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili, hawa jamaa wao ni akina nani katika taifa hili.

Mwogopeni Mungu enyi mafisadi na nyie akina Chiligati mnaowatetea mafisadi.

na Sadock Masusa, Tanzania, - 12.03.08 @ 11:42 | #1762

Chiligati, naomba unipe msimamo wa kisheria na katiba ya jamhuri ya muungano wa tanzania juu ya haya yafuatayo:-
1. Nini ni kosa la jinai?
2. Upotevu wa fedha za EPA unaconstitute kosa?
3. kama 2. hapo juu ni yes, je kosa hilo lina hadhi ya 'jinai'?
4. sheria za tanzania zinasemaje juu ya taratibu za kosa la wizi?
5. kwa mujibu wa mwanyika (jana) ''ni vigumu kuwajua individuals wamiliki wa makampuni hewa'' Vs bilioni 50+ zimerudishwa, chiligati unaelewa hilo? nani karudisha wakati mmiliki wa kampuni 'hewa' hajulikani? kwa nini azirudishe yeye wakati kampuni ni hewa?
mrudishaji analipa kwa niaba ya nani? uhusiano wao ni nini? nani huyo ajuaye moto wa EPA ulivyopamba bado akakubali kumlipia mmiliki wa kampuni hewa? je yeye si apprentice wa deal hilo hilo?
6. kama rais JMK aliridhika na ushahidi na uchunguzi wa Enrst & Young na kwa hasira zisizomithilika akatengeua ulaji wa Balali, kwa nini asiwape polisi hiyo report? polisi wetu hawana uwezo wa kukamata bank account za wamiliki invisible mpka hosea, mwanyika na tibaigana wapewe jukumu hilo?
7. inaelekea bank kuu wote hawajasoma topic ihusuyo ANNUITY, NET PRESENT VALUE, INTERNAL RATE OF RETURN, n.k. je wewe chiligati wajua kuwa hela huzaa japo riba sababu inatumika?
8. kama hiyi ni annual audited report ya 30 June 2006 (yaani mwaka wa fedha 2005/2006), interest rate inajulikana ya BOT, time (muda) inajulikana, cash iliyochukuliwa inajulikana inashindikana nini kupiga hesabu rahisi hivyo? au ndio ile list ya wale watoto wa wakubwa iliyotolewa na sauti ya watu last year wenye masters degree za kuchonga, wasioiva vema shuleni ili tu wajulikane wana elimi kutuzidi wengine?
9. chiligati, Kikwete anajichafua mwenyewe, hachafuliwi; kwa nini anachukua njia ya ajabu kukamata wezi?
10. labda nikuulize swali lililopaswa kuwa la tatu/nne hapo juu; chiligati kwa mtazamo wako, je waliochukua bilioni 153 BOT ni wezi?

11. kama ni wezi sehemu yao sio polisi, mahabusu na mahakami?
12. kwa nini tume ya mwanyika, hosea na tibaigana inachunguza uchunguzi wa Auditor, je hatutakuja kusikia kuwa balali kaonewa kutenguliwa ugavana?
13. chiligati, mwambie kikwete, hatuhitaji mzunguko huu, mwambie afanye yafuatayo:-
A: aipeleke ripoti ya Auditor central polisi.
B: atengue nafasi za hosea na mwanyika.
C: hakuna kampuni hewa hivyo brela wana majina ya waanzilishi wa kampuni hizo, wakamatwe bila kubembelezwa na wakamatwe kwa mtindo ule ule utumikao kuwakamata viongozi na wafuasi wa vyama pinzani kwa Chukua Chako Mapema (CCM)
D: kama asemavyo mwanyika kuwa sharaholders wa kampuni hizo hawajulikani basi BRELA wote wafukuzwe kazi kwa kusajili kampuni zisizo na majina ya wamiliki, na wabebeshwe pia hasara hii kwa taifa.
E: board ya wakurugenzi BOT (i don't know trustees, call it anything) iliyopita ishitakiwe kwa kukurugenzi upumbavu huu wa EPA tena kwa miaka yote hiyo. CV zao zisibaki na usafi ''eti muda wa bodi hiyo umeisha hivyo waziri wa fedha kachagua bodi mpya na rais kaassent''' ujinga huu hatuutaki.
F: You are all failures kwa kukwepa ukweli kuwa mwivi stahili yake ni jela tena kwa hawa ni jela ya mauti.

na bubu - 12.03.08 @ 11:57 | #1767

Those are the kicks of a dying Horse!CCM mtavuna mnachopanda.wacheni wa TZ tuseme angalau kwa kusema pressure inashuka.haingii akilini kuwa sisi walala hoi tuwekwe mahabusu lakini mafisadi wakae makwao na waombwe kurejesha mali walizokwepua kwa wakati wao.No!! whats so special with those guys?? yaani wao ni bora zaidi? wao ndiyo wa Tz hasa kuliko Umma..No p,se!

na Mlowe richard, DSm, - 12.03.08 @ 12:06 | #1768

Mheshimiwa Chiligati acha tuseme ukweli acha janja ya nyani.Hii ni issue ya kitaifa na sio ya CCM.Hivi kuna ubaya gani kutaja majina ya waliorudisha fedha.Wasiwasi wetu ni kwamba aidha hakuna fedha iliyorudishwa au baadhi ya wahusika wako katika kamati yenyewe ya EPA.Haiingii akilini kwamba waliorudisha fedha hawajulikani? Kama wamelipa kwa hundi si jina la mlipaji au kampuni yake inajulikana shida iko wapi.Mnataka kutuambia kwamba BoT haijui ilimlipa nani na kamati ya EPA haijui nani amerudisha hiki ni kituko cha karne.Naona kuna umuhimu wa kuongeza wajumbe wawili kwenye tume ya EPA nao ni Dr.Mwakyembe na Eng Stella Manyanya walioweza kumaliza kazi nzito na ya hatari kwa siku 45 tu wakati hawa wenzetu wa EPA wamemaliza siku 60 bado wanasuasua na kukwepa majukumu

E.Brown,Mwanjelwa,Mbeya

na Earnest Brown, Mbeya, - 12.03.08 @ 12:11 | #1780

Kutumia lugha chafu si nzuri kwa binadamu yoyote, awe rais au raia wa kawaida. Awe mtoto au mtu mzima. Wote wanastahiki lugha nzuri na kauli za busara.

Tukija katika hali inayoendelea Tanzania ya ufisadi, raia yoyote mwenye akili timamu na kuipenda nchi yake na watu wake haachi kujiuliza masuala mengi katika hii hali ya ufisadi uliogundulika na unaoendelea kuchunguzwa.

Baadhi ya masuala ambayo watu wengi yawapitikia: je ni kweli Tanzania kuna sheria za kuwanasa mafisadi kama hao tulionao. Katika hali inayoendelea, haiwezakani mtu afanye ufisadi kama huo halafu aweze kutanua na kudunda mitaani bila kukamatwa kisheria na kuburuzwa mahakani. Kadhia ya Richmond sisi inatusikitisha kuwa mpaka sasa hakuna mtu aliyefikishwa mahakamani na wahusika wanadunda mitaani na biashara zao kama kawaida. Sijuwi hapa mtu atasemaje, bado ni ushabiki wa kisiasa tu. Kadhia ambayo kila mtanzania anakamuliwa milioni 3.8 kwa siku hali ya kuwa raia wengine hawana hata kula yao ya siku moja, halafu useme watu hawana subra. Naomba tuweni na hisia na wengine, Taifa na ubinadamu.

Kadhia ya BOT, vile vile inasikitisha pamoja na kazi nzuri aliyoianzisha mheshimiwa Rais. Sisi wengine, pengine hatuzijuwi sheria vizuri, inatusikitisha kuona mtuhumiwa wa wizi na kurehejesha alichoiba bila kutiwa mbaroni na kufikishwa mahkamani na kuisaidia polisi katika uchunguzi. Hapa wengine hatuoni mantiki pamoja na kuwa suala bado limo katika uchunguzi. Hawa waliorejeshwa wakiachiwa bila kukamtwa hivi sasa basi wataharibu uchunguzi wote, kwa hivyo kulikuwa na umuhimu na kudhibitiwa na vyombo vya ulinzi.

Bila kukamatwa watuhumiwa hao na wengine ufisadi utaendelea, uchunguzi utaharibiwa na raia watapoteza imani na uongozi wa Serikali iliyopo


Hayo nia maoni machache tu. Ninayo mengi kuhusu kadhi hizi.

na Ali, Tanzania, - 12.03.08 @ 12:19 | #1782

kwa nini Mwanyika ajiuzuru na huku pesa walitumia watu wengine kwenye uchaguzi. Yeye kachaguliwa tu juzi juzi, kwanini msimseme Chenge aliyekuwapo. Ajiuzuru aende kula nini na watoto wake ambapo waliokula ni kuanzia TOP. Mwacheni Mwanyika huyu ni sisimizi kuna wale vinara wenyewe wanaohusika.

na maggy, tz, - 12.03.08 @ 12:35 | #1787

mimi nafikiri suala liko wazi tena sana, Napenda Chiligati aelewe kuwa (km alikuwa hajui!!!) tuko katika MAPAMBANO na
katika kupambana, wapo watakaolia, kuhuzunika, na hata wapo wanaopoteza maisha kutokana na athari za mapambano jambo ambalo ni la kawaida, lakini hali hiyo HAISIMAMISHI mapambano kwani lengo ni kufanikisha lile lililokusudiwa kufanywa.
Kwa mantiki hiyo katika mapambano ambayo tumo ya ufisadi baina ya serikali vs wananchi – wapo watakaoathirika ikiwa ni upande wa viongozi (wa CCM hasa) na wananchi (bila kujali itikadi zetu kisiasa), lakini kamwe hatuwezi kusimamisha vita hii wameianzisha wenyewe ikiwa na maana wako tayari ku…… Hazushiwi/kuchafuliwa wala kusifiwa mtu hapa ni Tanzania ndio imeshushiwa HADHI. Lazima watanzania tupambane kurudisha hadhi ya nchi yetu.

Hapa ni asubuhi bado tunajipanga, mpambano wenyewe bado kuanza, kwani ikijafika mchana kama si jioni, tayari tutakuwa tumeshaikomboa Tanzania yetu, tukiwa na majeruhi kama si marehemu kadhaa! Hilo bwana Chiligati unatakiwa achilia mbali kuliewa bali kuliweka akilini.

Mungu tubariki watanzania wenye moyo wa kuikomboa taifa yetu!

na AA, Moshi, - 12.03.08 @ 12:37 | #1789

NDIYO,Rais kukaa kimya ni sehemu ya ufisadi.Yaani huyo Chiligati anaona uchungu na neno uhuni? kwanza asitafsiri ustaarabu vibaya,hivi siku wananchi watakapoamua kuipindua serikali seriously kwa vitendo atasema nini?

Who will respect JK as the president if he doesnt respect himself?wananchi walimheshimu wakampa mandate ya kuongoza but Mr chosen to hurt the citizens providing protection to corrupt leaders,exploiters and expert burgeous.I cant respect such kind of a person but by the influence of my patriotism i'll have a respect to presidential office not JK as the president

Kwanza Chiligati akae chini kwanza atafakari yeye kama chiligati ameweza vipi kulisaidia taifa hili maskini kupiga hatua kimaendeleo.Huyo namfanananisha tu na huyo mkuu wa jeshi wa Zimbabwe anaesema hata Mugabe akishindwa uchaguzi watapindua serikali.Damn!

na Ben, India, - 12.03.08 @ 13:05 | #1798

Mdanganyika usidhani kuandika maneno yasiyo ya kistaarabu ndio uanaharakati! kwa kauli zako tuu mwenye akili yeyote hataacha kuamini kuwa wewe ni mpungufu wa malezi bora.MBOWE unaendelea kuwa kikwazo cha kukua kwa upinzani nchini kwa kuwa umeshindwa kuwa mstaarabu wa kupingana kwa hoja na UMEKUWA UKITOA LUGHA ZA DHARAU, MATUSI NA UBABE as if Watanzania wote hawana akili za kupambanua.
TUTAKUADHIBU ZAIDI 2010.

na POLI, DAR, - 12.03.08 @ 13:09 | #1800

Poleni sana wa-Tanzania wenzangu kwa shida tunazozipata kila siku. Naamini mojawapo ya waliotuletea shida hizo ni hao mafisadi/wenye-CCM.

Kwa hakika hapa Tanzania hakuna jinsi unavyoweza kuongelea ufisadi bila kuihusisha CCM. Kwa maneno mengine ufisadi na CCM ni sawa na Mtoto na baba. Baba wa ufisadi ni mweyekiti wa CCM. Kukaa tukapiga kelele za ufisadi bila kuingoa CCM madarakani ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu.

Hivi kuna M-Tanzania asiyejua kuwa bila huo ufisadi tunaouongelea kila siku CCM isingekuwa madarakani. Kama kweli CCM wana nia ya dhati ya kuendelea kuwa madarakani hawawezi kuachana na ufisadi. Hili nalitamka nikiwa na uhakika mkubwa. Hizi porojo za ufisadi tutapiga sana mpaka tuchoke kama haturudi nyuma tukafikiria jinsi ya kufanya.

Mimi nawashauri watu wetu wenye vipaji kama kina Dr. Slaa, wakiri makini na maarufu Bw. Tundu Lissu na Mheshimiwa Mbowe wafungue Account katika banki mbalimbali tuwawekee pesa wazunguke nchi nzima bila kuchoka wawaelezee wananchi chanzo cha umaskini wao wanaoteseka nao kila siku na nini wafanye. Naamini kwa kufanya hivyo CCM tunaweza kuingoa.

Tukishawaelimisha wananchi nd'o tuingie barabarani kudai tume huru ya uchaguzi. Hii utakuwa ni mwanzo mzuri wa wapinzani kuingia ikulu. CCM ikiondoka madarani ufisadi labda unaweza kubaki kama historia.

Nawasii watanzania wenzangu tufikirie kwa mapana na marefu hayo niliyoyasema hapo juu ili tuinusuru nchi yetu na CCM/Ufisadi. Imefika hatua kutaja neno CCM hakuna tofauti na kutaja neno fisadi.

Bila kuchukua hatua madhubuti tutaendelea kupiga soga za ufisadi kila kukicha huku wao wakiendelea kutanua.

na Rutagatina Regemalira, Safarini Finland, - 12.03.08 @ 13:30 | #1802

kashifa yeyote dhidi ya serikali iliyoko madarakani ni mtaji kwa wapinzani duniani kote,hivyo nijukumu la CCM kuhakikisha watu wanaopewa dhamana ya kuongoza nchi/taasisi mbalimabali siyo mafisadi.

CCM ijue kuunda tume ni kitu kimoja na kuchukua hatua kwa waliohusika ni kitu kingine, wananchi wanachotaka ni kuona hatua zinachukuliwa.

Kama walivyo watuhumiwa wengine wanaoswekwa rumande wakati uchunguzi unaendelea ili wasiharibu ushaidi, mpona hawa wanaorejesha fedha za EPA, awapelekwi keko/ukonga/ segerea???????

na Billy - 12.03.08 @ 13:33 | #1806

nakushangaa kaptein Chiligati kwa kutumika kama mashine ambayo kwayohaina akili ya kufanya upembuzi zaidi ya kusukumwa na anayeiendesha.

pengine ujeshi wako umesababisha athari hizo, haiingi akilini kwa mtu kama wewe kugeuza ishu ya EPA kuwa ya CCM na Upinzani.

tunaanza kukukusanya kumbukumbu ya masuala kadhaa uliyowahi kuyatekeleza huko nyuma na kupatwa wasiwasi na kile unachokitekeleza, suala kubwa la hivi karibui likiwa ni hatua yako ya kutangaza mishahara iliyozua kashehe

hakuna sababu za kumtetea Kikwete mwambie wananchi wanataka kumwona daudi Ballali amefikishwa mahakamani pamoja na wote waliohusika kufuja bilioni 133 za watanzania

watanznaia tunasema kwmaba hakuna lugha nzuri inayoweza kutumika kuelezea suala hili zaidi ya kuwafikisha mahakamani wahusika badala ya usanii unaofanyika hivi sasa

Mashilatu, Ngara

na Mashilatu, Ngara, - 12.03.08 @ 13:38 | #1809

Andika kwa maneno yoyote yale mambo ndio hivyo.Mbowe aseme au wananchi walie it does not matter.Pesa ya EPA zimeishaliwa,za richmond zimeshaliwa na zingine zinaendelea kuliwa na zingine zitaliwa miaka ijayo lakini hakuna kitachoendelea.
Sawa mafisadi wa EPA au richmond wanafahamika lakini hawachukuiliwi hatua-Kwa nini?Mpaka hapo mbowe na wengineo wanaopiga domo hawajaelewa?
Mbowe na wenzake ni vinyonya nguvu kwasababu wanasema mambo ambayo hawayaelewi vizuri and they cannot do anything about it.
Bamboligo,Dar

na Kingsley, Dar es salaam, - 12.03.08 @ 13:47 | #1815

MMhhhhhhhhh,

watanzania mnapenda sana kudakia mambo msiyoyajua, kweli katika mawazo yenu mnafikiria Rais Kikwete atakaa kimya bila kutaja majina ya waliohusika na ufisadi au hatawachukulia sheria????????? Au mnaongea tu kwasababu mmepewa uhuru wa kuongea?

Rais Kikwete ni mtu asiyependa kupaparika na mambo, anafanya mambo yake taratibu na kwamakini ili akitoa taarifa atoe taarifa zilizo sahihi. Mbowe hujakomaa Kisiasa kabisa, tena haufai kabisa kuwa Rais maana unapotosha Jamii, kama wewe ni mwanasiasa uliyekomaa, ulipaswa kuuliza ni kitu gani kinaendelea kuhusiana na kashfa hiyo ya EPA sio kuanza kutoa conclution zako ambazo leo hii ukiambiwa uzijustify utashindwa. Unaushahidi gani kuwa Raisi Kikwete anahusika na Kashfa hiyo? Au unaongea tu ili kujiwekea jina na kumchafulia jina mwenzako? usitafute sifa kupitia jina la mwenzako, fight on ur own men. Tunaomba katika kampeni mtoe sera zenu sio kuanza kuongelea mabaya yaliyofanywa na CCM ili nyie muonekane wazuri. Nina uhakika hata nyie mngekuwa serikalini, kungekuwa na kashfa nyingi tu kama hizi, hakuna binadamu ambaye yuko perfect, so msitumie nafasi hizi kujionyesha kwa watu nyie ni bora zaidi, kumbe nyie mnaweza kuwa wachafu zaidi ya hawa. "Toa Boriti kwenye jicho lako ndio utoe kibanzi kwenye jicho la mwenzio"

Tanzanians, Please be patient, and see what measures will be taken to all these wafisadi, Tusiharibu amani tuliyonayo Tanzania.

na Asia, Tanzania, - 12.03.08 @ 13:47 | #1816

Hawa kina Chiligati wananunua kesi zisizo zao. Mtakuja kufa muda si wenu. Watanzania wamechoka na usanii wa JK, uhuni wa kutufanya hatuna akili. Hela mle kwenye kampeni za CCM, mlidhani yatafichika. Miaka hii si ya YES MAN. Tuna macho na tutawamulika mpaka uvunguni mwenu kina Chiligati. Ubabe wenu na Kingunge wenu wa kujibu hoja kwa jazba na vitisho havisikilizwi saa hizi. Kinachotakiwa ni ukweli mezani. Nani aliwaambia TZ ni ya CCM, mafisadi wakubwa nyie.

na Karamagi, Dar, - 12.03.08 @ 13:52 | #1818

Nimeshasema kwamba kwa mtaji huu, CCM itaendelea kuongoza kwa miongo mingi ijayo kwa sababu ya aina ya viongozi wa upinzani tulio nao. Ni bora hivi vyama vya siasa vingefutwa. Ni wababaishaji kuliko hata hao CCM wenyewe.

na majungu, Muleba/Tanzania, - 12.03.08 @ 14:21 | #1830

Upinzani unajua unachokifanya. Unajua fika kwamba nyuma ya pazia la EPA kuna mwali anaitwa CCM. Kelele za upinzani kuhusu EPA una nia ya kuonyesha mkono wa CCM katika sakata hili. Tangu hapo EPA ni siasa na asiyetaka kukubali hilo ajue kwamba hajui nini kinaendelea katika mchezo huu.

na Byase, Dar Es Salaam, - 12.03.08 @ 14:32 | #1833

Bwana KADAGO kutoka mwanza wewe ni kada nini??toka umeishi hapo nyumbani ulishaona mwizi anaundiwa tume?!na wizi wenzake!!acha bwana simama kwenye ukweli,au ulishaona mwizi anabembelezwa kurudisha pesa alizoiba nenda mahakama ya kisutu uone mwizi wa kuku anafungwa miaka mingapi,halafu unajua kinacho kosesha imani na hiyo tume umemsikia juzi MWANYIKA kasemje(AJABU KWELI BONGO)eti makampuni yaliyochukuwa pesa yanajulikana ila watu wa hayo makampuni(wamiliki)hawajulikani unasikia UHUNI wa huyo mwanasheria wetu,sasa hizo pesa wakinani wanazirudisha jamani,!!halafu kadago unataka kutuambia nini tuwape muda wa kufanya nini??? kwanza HOSEA ,MWANYIKA WOTE SI WASAFI URICHMOND UMO NDANI YAO si huyo HOSEA alisema mkataba wa kampuni ambayo haijui hata kuweka Balbu WALA HAIPO KATIKA DUNIA HII(RICHMOND)ulikuwa halali hauna mashaka yoyote,IZENGO KADAGO nakujua toka uko RTD enzi hizo nakuheshimu,usije ukapoteza mwelekeo kaaa kimya tafadhari

na simba, athens greece, - 12.03.08 @ 14:35 | #1835


Haingiiii akilini kabisaaaa kabisaaaa eti mbowe anakurupuka si kweli mnasema hivyo sababu ninyi ni walevi wa siasa za danganyika.

Mbowe chama chake kimechangia 100% kutufungua macho wadanganyika kufikia hapo tulipo fika JK hana ujanja wa kushindana na nguvu za wakati namsifu ni mwerevu ndo sababu anaruhusu mijadala kama hii.

Zito kabwe alifukuzwa kimizengwe Bungeni matokeo yake wabunge kuzomewa ni Chadema huyu, JK kamteua kwenye kamati ya madini alijua si mwongo kwani angekuwa mwongo asingemteua na yule aliyemtuhumu Waziri NK yuko wapi sasa?

Dr Slaa pale mwembe yanga alitaja listi ya 11 pax, baadhi walidai wanakwenda mahakamani ni aibu kubwa kwani sijawasikia mahakama waloenda ni ipi? au ni ile ya Charles Tylor? pia aliibua EPA lakini Balali yuko wapi AIBU? uvumilivu upi nchi imevunda kundi la wachache linaishi peponi na walio wengi tunakufa kihoro,hata nauli ya daladala hatuna ni kwat kilomita 50 kila siku. IPTL na RICHMOND kila siku Tanesco inalipa Shs 300,000,000.00

Inashangaza sana kama si kutia kichefuchefu mtu na akili zake akitetea na kumlaumu Mbowe.

Mbowe ni kijana Tajiri alizaliwa ukoo tajiri na ameendeleza utajiri hou. lakini ana karama,kipaji wito wa kutetea maslahi ya wanyonge badala ya kung'ang'ania mali za umma wa watanzania aliachia hata ubunge ambao vigogo wengine ni wabunge wa miaka mingi lakini bado wanang'an'gania sababu ya maslahi yao matumbo yao.

Juzi mbunge mmoja wakilosa aliyekuwa waziri mwandamizi wa mipango alichana live eti watu wasikodolee macho jimbo lake hii kwani ni mali binafsi.

Uchungu wangu ni mwingi.

Ila nasema kwa ufupi Mbowe big up usilegeze uzi kabisaa tupo pamoja nawe.

na mossi, dar-es-salaam,Tanzania, - 12.03.08 @ 15:02 | #1841

Katika jukwaa la kujadili mambo mengi ya kitaifa, watanzania tumekuwa watu wepesi wa kusahau. Nadhani tunahitaji kuweka kumbukumbu ya yote yaliyofanyika ambayo tunahitaji majibu. Tusiwe tunapelekwa kwa upepo. Juzi lilikuwa la rada na ndege (hakuna suluhisho),jana la list ya mafisadi+ balali+richmond (hakuna suluhisho), leo la EPA(hakuna suluhisho), kesho sijui kitakuwa nini?

Kuna haja ya taasisi zisizokuwa za kisiasa kushiriki kikamilifu kutoa elimu ya urai Tanzania, ili mijini na vijijini watu waelewe, waweze kudai na kutetea haki zao, wasisubiri tu kudangwanywa wakati wa siasa na wasijazwe propaganda za siasa. Ni watz wachache wanao elewa nini wajibu wa serikali kwao. Mara nyingi wanaona kuwa chochote kinachofanywa na serikali katika maeneo yao ni upendeleo; mathalan, utaona jinsi mijini na vijijini wanavyofurahia misururu mirefu ya magari ya kifahari ya watawala wakati watoto wao hawana madawati, huduma za afya n.k. Haya ndiyo yanayofanya wengine kuhoji "kama ungekuwa upinzani usingefanya hivi au vile", swala sio chama, ila ni haki ya kiraia, kwani kila chama sera yake ni kuwaletea rai maendeleo yao, kama zilivyo dini kuwa ni kuwapeleka ahera waumini wao. Leo utamwambia nani aandamane, wakati hajui kanyimwa kitu gani?

Kuna mengi sana ya kuisemea Tanzania, kwani uelewa mdogo hasa wa haki za kiraia wa WaTz umekuwa mtaji mkubwa wa wanasiasa hasa kwa waliopo madarakani. Nadhani tunahitaji kufikia mahali tuseme nani, na anauwezo gani kuiletea nchi maendeleo na sio kubaki huyu ni mwenzetu! Naamini tukiweka uzalendo mbele, tunaweza kuiletea nchi yetu mafanikio kabla ya miaka 100 ambayo CCM inaamini itaendelea kuwa madarakani.

na Paul, DK, - 12.03.08 @ 15:10 | #1843

Hi HUYU chilligati zimo kweli!!!
Namwomba ajiweke ktk hali ya mwananchi wa kawaida,afikilie vizuri maneno ya huyo m-kiti wake wa chama akimwambia haya katika hali ngumu ya sasa.Alikuwa waziri wa ajira juzi juzi tu hapa mara kapandisha mishahara,wadhamini wa chama chama chake wakamshika masikio akashusha.Ktk hali hiyo mwenyekiti wa chama(kwani ni rais ktk kutetea masilahi ya mafisadi walomchangia ktk kampeni)Anatoa matamko tuuuu..
-MAJINA YA WALA RUSHWA NINAYO WAJIANDAE
-MAJAMBAZI WAJIANDAE(HAT MAKAMU WAKE JUZI KASEMA HIVYO)
-LOWASSA KAPATWA NA AJARI YA KISIASA(NAYE ANAJIANDAA)
Yaani amekuwa raisi wa matamko tu mpaka lini?Nahisi hata hayo majina yanayofichwa ya EPA,lake limo(ajari ya kisiasa).Nadhani tulijidanganya kwa tabasamu lake,mpaka naona ni bor hata huyo aliye mjasiliamali wa ikulu,kwani hakuw na muda na wananchi.Huyu mwekiti wa chama tatizo hana msimamo,mwema na mbaya wote wake,ITS POPO LIKE!!!!!!!!!!!!

na KIMUNE, dar, - 12.03.08 @ 15:13 | #1844

Sipendi pale Chiligati anapokuwa msemaji wa Kikwete,jipange upya usiwe mhariri wa watu.TUMECHOKA.

na mnyonge, musoma, - 12.03.08 @ 15:21 | #1846

Nataka kusema kitu lakini huyu bubu # 1767 amejifunza kusema niliyotaka kusema ingawa tungetofautiana ufikishaji! Mh. Chiligati mbona unaanza kuwa chilli? Umekuwa Waziai mshika dau wa mambo ya kutekeleza sheria pale mambo ya ndani, hata kama ulikuwa bado hujapitia pitia kabla lakini baada ya kufika hapo utakuwa umepata mbinu moja au mbili za utendaji wa makosa ya jinai. Ile tume ya EPA ina Mwanasheria mkuu, JPM, Mkurugenzi wa TAKUKURU, EH, Inspekta Jenerali, SM, hawa jamaa wote wanakumbukwa pale UDSM kwa umahiri wao, Mwema ametolewa Nairobi akiwa Interpol regional bureau, ni mtaalamu huyu, je wote hawajui kama watuhumiwa hukamatwa na kutiwa ndani ili kusaidia uchunguzi? Mwanyika ametuambia kama watuhumiwa wa EPA wanarudisha mapesa, pesa zinarudi vipi bila wahusika kuandika nyaraka za malipo? Pesa zinakuja ktk hewa na kuingia ktk akaunti za BoT? Waache utani na watu wazima bwana! Huyu Mwanyika na Dr Hosea kichwa ngumu sana, wafanye kitu basi ili watanzania waseme sasa bravo. Kutapika kunakera hata kwa mgonjwa mwenyewe,anayemhudumia atamuonea huruma, lakini kujipakaza matapishi inakosa maelezo! Hawa jamaa wametakiwa kuondoka na kama wameshindwa nafikiri ni wakati muafaka wakaondoka.
Kwa Mh Chilli aone kulikuwa na sababu ya Rais kuonesha uchungu wa kilichotoikea nchi yake na wananchi wake. Kipenzi chake kimeondoka ameonesha kutokufurahia jambo hilo kwani aliendelea kumpamba lakini mweleka ambao Lowasa amempiga tena ni kukiri kuwa alijua kama mkataba wa Richmond ulikuwa na makosa na bado aliuruhusu ufanye kazi. Ni huyu ambaye alimpa taarifa zilizomfanya Rais alihutubie taifa na kuwaeleza mambo kuhusu umeme yatakuwa safi, bado hajakemea na kuonesha kusikitikia hilo pia, sasa asihusishwe vipi? Kama Lowasa alihusishwa kwa uwajibikaji basi na Rais yumo pia. Bado Rais anatuambia tusahau hayo kwani ni utelezi tu katika siasa, ni kweli Mh Chilli hiyo inakaa sawa akilini? Mimi nilifikiri hata ingejadiliwa mimi kurudishiwa kiasi cha pesa za gharama za umeme kwani nimelipia hata ule nisioutumia. Mbaya zaidi tunajua sasa kwamba hata hizo pesa tumekuwa tukiichangishwa kwa ajili ya watu wachache. Zile za EPA ni pamoja na chama tawala kugaharimia kampeni za uchaguzi. Tuhurumie Mh Chilli, mwambie Mwenyekiti wako aseme kitu cha kuturudishia imani yetu kwake, asione watu hawa ni mbumbumbu. Uwanja wa mchezo huu umekuwa mkubwa sana huwezi kucheza sehemu zote.

na Christopher, Dar - Tz, - 12.03.08 @ 15:25 | #1848

Sijui ccm wanataka watu waeleweje Rais kushindwa kutumia mamlaka aliyonayo kuwachukulia hatua stahiki watuhumiwa huku akiwajua kabisa,au anataka tukae kimya ili kumfurahisha,ila hatuwezi kushabikia ufisadi juu ya ufisadi,,mbowe amefanya jambo la busara na la kuungwa mkono,
Ephata

na Ephata, Arusha, - 12.03.08 @ 15:57 | #1855

Swala la ufisadi nchini Tanzania ni lazima liangaliwe kwa mtazamo mpana zaidi kwani linatia doa taifa na hao mafisadi wanao rudisha fedha hio wawekwe bayana hakuna haja yakuendelea kuwaficha na hatua kali dhidi yao zichukuliwe.Mheshimiwa Rais bado tuna imani kubwa sana nawe maneno yawapinzani yasikutie shaka.

na Saitoty olle, Kampala Uganda, - 12.03.08 @ 16:28 | #1860

Asia lazima kuna jambo, sauti ya wengi ni sauti ya Mungu, wote waliochangia wako kinyume na wewe, je wote hawa hawana akili?? ata wewe kabla ya kuwaeleza watu watoe boriti je hawa na marais??je wewe umetoa boriti la kuwaambia wenzako wanapapalika??WEWE MTU LOWASA ANGEJIUZULU BILA WATU KUPIGA KELELE,uko dunia gani wewe, wanakupa sh ngapi kuwatetea??

na Imani Martini, usa, - 12.03.08 @ 16:34 | #1865

Kuna usemi usemao "tell me who is your friend,I'll tell you who you are.WHO IS THE CLOSED FRIEND OF JK?Lowassa?Rostam?Or Mtikila?jibu unalo
Ni ambie nani rafikiyo nitakuambia wewe ni nani.Rais amewekwa kukitumikia interest za nchi ,kila nchi ina interest zake km ilivyo USA in Iraq,Kashmir in India & Pakistan.Km President akishindwa kulinda maslahi ya taifa hapo ndio minong'ono na maneno ya hasira huanza hata kusababisha wananchi kumg'oa madarakani e.g Georgia,Ex Yugoslavia n.k.Niwakumbushe wakati wapinzani walivyo piga kelele kuhusu Ufisadi KIBABU Kingunge Ngombare Kilikuja juu huku chenyewe kikijua kimejilimbikizia mali Hata Kutoa Maneno ya kejeli kua wapinzani hawana sera .lkn wote tumeona yaliyotokea CCM.Napenda kumtahadharisha Captain John K.Atoe maoni kwenye A.K 47 au tanks aache wanasheria,wachumi wafanye vitu vyao.Asimuige KIBABU KINGUNGE.PIa nchi za wenzetu Rais anapo apishwa huachana na chama ili kuwa neutral kwa maswala ya kitaifa.

na sina jina, P.R.CHINA, - 12.03.08 @ 17:04 | #1873

nashukuru mr Poli,ndo raha ya ukweli inpomuingia muhusika lazma aumie,na kwa sisi watu wa human and social psychology tunajua nini wasiwasi wako.Hakuna ubishi mabilioni ya EPA yana uhusiano mkubwa sana na CCM!!!ACHILIA MBALI MAGALI YAILYOLETWA WAKATI WA UCHAGUZI KILA MKOA NA WILAYA YALIYOANDIKWA "HUNDRA"!PIGA HESABU ZA GHALAMA YA WASANII WA BONGO FLEVA WALOZUNGUKA NA JK NCHI NZIMA,VICK KAMATA ALIYEMMIMBIA WIMBO NA KUMFANANISHA JK NA NABII SULEIMAN SASA YUKO B.O.T,NGWEA NA WIMBO WAKE WA MTOTO WA JAKAYA,NA KAMPUNI YA GHAFLA YENYE KUTENGENEZA MASHATI YALIYOANDIKWA "JAH-KAYA"[sijui ata ilipopotelea hiyo lebo}WOTE HAWA WALIITAJI HELA UNAFIKILI ZIMETOKA WAPI?MKUMBUKE KOMBA NA GARI LAKE NA,K-LYN,ACHILIA MBALI BUSHOKE ALIYELUBUNIWA ILI WIMBO WAKE WA "msela jela"ALIOIMBA KWA AJILI YA BABU SEYA NA RAFIKI YAKE PAPII KOCHA USPIGWE RADIONI,BUSHOKE ALIANZSHA HARAKATI ZA KUMTOA BABU SEYA GEREZANI KWA NJIA YA WIMBO SABABU KESI YA BABU SEYA INAHUSISHWA NA J.K MPAKA KESHO,LAKINI ALITULIZWA KWA HELA ZA KAMPENI TOKA B.O.T!!HUU NDO USANII WA J.K NA NDO MANA ISHU ZA B.O.T ANATAKA KUZIPELEKA KISANII!!DEEP GREEN NI MALI YA C.C.M!!ILIGHARAMIA KAMPENI ZOTE ZA C.C.M 2005!!!!NASEMA IPO SIKU,WHEN ZE GROLY OF GREEN AND YELLOW COLOUR WILL TURN TO LITRES OF TEARS AND RIVERS OF BLOO!!KIPINDI AMBAPO MUNGU WA HASIRA WA AGANO LA KALE ATAKAPOWARUDIA WATZ,YULE MUNGU ALIYE WAUA WAMISRI NDANI YA BAHARI YA SHAMU,MUNGU WA KISASI,ALIYEMNYIMA MUSSA HAKI YA KUONA NCHI YA AHADI WAKATI NDIYE ALIKUWA NABII WAKE ALIYEMTUMA MISRI,MUNGU WA HASIRA ILIYEWATUPILIZA MBALI WATU WA SODOMA NA GOMORA KWA MOTO WA KISASI,NDIYE YULE ALIYEJITOKEZA KWA MUSSA KTK KICHAKA CHA MOTO AKIONYESHA UKALI WA MATENDO YAKE ULIVO KAMA MOTO,MUNGU ALIYETUMA GHARIKA KWA NUHU!!!TUNAHITAJI TABIA HIZI ZA MUNGU HUYU,HUYU ALIKUWANI MUNGU WA KUNUNA ALIPOKOSEWA!!!HATUMTAKI MUNGU WA AGANO JIPYA KWA HALI YA SASA TANZANIA HII,MUNGU ALIYEKUJA KUHIMIZA UPENDO HATA KAMA UNAIIBIWA NA MAFISADI,MUNGU ANAYESISITIZA KUWA AKUPIGAYE SHAVU LA KUSHOTO MGEUZIE LA KULIA,MUNGU ANAYESISITIZA KUWA AKUNYANG'ANYAE KANZU MPE NA JOHO,AKUOMBAYE UMSINDKIZE MILE 30 WE MSINDIKIZE MILE 60,ATUKUBALI CCM ITUPIGE KUSHOTO SI TUIPE KULIA,TUISINDIKIZE KUFIKA IKULU ITAKE TUISINDIKZE KULEA UFISADI,IIBE HAKI ZETU NASI TUIONGEZEE MALI ZETU!!!AM A COMING CONSERVATIVE DELAYED IDIOT,I'LL NEVER BE SHAKED WHEN MY TIME REACH TOM MAKE CHANGES TO MY "DEAR MAMA TANZANIA"j.k acha usanii rudisha hela zetu za EPA!!!

na mdanganyika, tz, - 12.03.08 @ 17:22 | #1879

Asia unajua unachoongea au wewe ndio umekurupuka kudandia usilolijua mama??au sijui dada yetu!??sisi tuko nje lakini mambo ya nyumbani tunafuatilia wewe uko Bongo hujui UFISADI ni kitu gani sikiliza dada,mimi siyo msemaji wa watu ila kwa taarifa yako Bwana Mboe hawezi kutafuta umaarufu kwa kupitia jina la Mh Rais kikwete sawa mama!! mboe tunamjua miaka nenda miaka rudi toka enzi za kucheza disco upo hapo!!(nafikiri ulikuwa mdogo au hujaja mjini) kikwete nyota yake imekaa mwaka 1995,wakati mboe tunamjua sawa wewe mtoto wa kike!! ila mboe ni mzalendo ndio maana anapiga kelele,hana njaa yule jamaa uelewe kwanza likae akilini,(simpigii kampeni) au dada unata kugombea nafasi ya mwenekiti ccm vijana??(AMINA CHIFUPA YUKO WAPI!!)hata kampeni haziwi hivyo sawa dada tunakuheshimu hujui nyamaza,wewe unasema Rais Kikwete mtu makini siyo unajua alihidi nyumba walizouziwa viongozi zitarudishwa anamiaka miwili ikulu hata yake hajairudisha alisema majina ya wala rushwa anayo ila anawapa muda wajirekebishe!! majina ya wauza unga anayo lakini kayakalia ikulu,huyo ndio makini siyo dada!!SIKILIZA WEWE DADA ASIA FUNGA DOMO TAFADHARI UNATIA KICHEFUCHEFU SAWA!

na Tinoh, athens greece, - 12.03.08 @ 17:27 | #1881

kinachonisikitisha ni kwamba haya maoni yote wananchi wakawaida watayasoma?ambao hawana uwezo wa kupata huduma ya mtandao.ombi langu kwa ndugu mhariri utufanyie hisani uyaandike kwenye gazeti lako haya maoni ambayo ni changamoto kwetu sote watanzania hasa ya ndugu bubu.safari bado ni ndefu,lakini mwanga umeanza kuangaza

na binkwatileki, china, - 12.03.08 @ 17:31 | #1882

CHLILIGATI ACHA SIASA RUDI HARAKA TENA HARAKA SANA JESHINI

na MJASIA, IKULU, - 12.03.08 @ 17:32 | #1883

WANZANIA LAZIMA MJUE KUNA NATURAL PERSON NA ARTIFICIAL PERSON...SASA KWAMUDA MFUPI TULIOCHUNGUZA TUMENGUNDUA HAWA NI ARTIFICIAL PERSON.MTUWIE RADHI KIDOGO MSITUSUMBUE SANA MUWE NA ADABU NA VIONGOZI WENU...YANI HAMNA ADABU MNATAKA HAWA WAKALALE UKONGA?NO NO KABISA LABDA KAMA KUMEANZISHWA MAKAZI YA VIONGOZI UKONGA.HEBU MSILETE MAWAZO YA KIJINGA HAPA KATIKA HILI...KULE NI KWA WALALAHOI SIO WATU NA HELA ZAO.MKOME KABISA

na HOSEA, TUMENI, - 12.03.08 @ 18:23 | #1888


Ushabiki ni ugonjwa mbaya!! Kuna mtu katika kumtetea Mheshimiwa Rais amesema kwamba wapinzani waondoe boriti kwenye macho yao kwanza ... Huu ni ushabiki mbaya.

Swala hapa sio kumtetea mtu au kumdhalilisha mtu. Ni kusema yale yanayoonekana hata kwa kipofu. Kinachofanyika kinaonekana na kischofanyika kinaonekana.

Kwa taarifa yake huyu jamaa, kama wapinzani hawawezi kukosoa misimamo ya watawala basi hawana kazi yoyote katika jamii na hawastahili kuwepo. Na kama si hivyo kwa nini waitwe wapinzani, wanapinga nini?

Wapinzani hawana boriti la kutoa machoni kwani halijaingia bado. Watawala wao tayari wanalo hilo boriti na kila mmoja analiona. Kuwataka wapinzani watoe lao kwanza ni sawasawa na kusema kwamba hawana haki ya kuwapinga watawala!! Na boriti lao mpaka nao waingie kwenye utawala!!

Kwa mtaji huu, basi tukubaliane kwamba watawala wamechemsha na ni haki ya wananchi kuwasema na kuwaanika. Na Mbowe akiingia Ikulu itakuwa ni zamu ya JK kumsema na kumuanika. Na yeye awe na subira tu!!

Watanzania wanataka hela iliyooibiwa irudishwe pamoja na faida (riba), wahusika waanikwe waziwazi, halafu wafikishwe kwenye vyombo vya sheria. Hawataki usiri wala danganya toto. BASI.

na Amk, dar, - 12.03.08 @ 18:36 | #1890

dada asia unadandia treni kwa mbele,shauri yako hii treni inaenda zenji sasa kwa taarifa yako,ila si ajabu nilisema juzi ya kua wale wote ambao wazee wao,ama wao wenyewe ni mafisadi na wanapata pesa kirahisi km za richmond,hawawezi kusema lolote against jk na watu wake wa karibu katoka mkapa na kikundi cha watu wachache waliojinufaisha sasa kaja mwingine na kundi lake la kujinufaisha sikiliza asia,kosa ni kosa tu hata likipewa jina zuri vipi litabaki kua kosa,eti lowassa kapata ajali ya kisiasa kwa hyo mwizi wa mabilioni anapambwa na kupewa majina mazuri,mi simkubali kikwete tokea hiyo 1995 na alipokosa nilifanya sherehe kivyangu ila nilijua anarudi na kufanikiwa hasa baada ya baba wa taifa kufariki,sikua na lakufanya tu kumzuia,na kabla sijaondoka kuja huku nilipo kimasomo nilikua nabishana sana wale wote waliokua wanampenda kisa ana mvuto as if mvuto ndio unaongoza nchi,ila niliwaambia ya kua baada ya muda wananiandikia na kunipigia simu kuniambia,na mwaka jana mwanzoni walianza kuniandikia na kulalamika jibu langu lilikua ni mapema mno kulalamika kwani yapo mengi ya ajabu ambayo kikwete atayafanya yatawaudhi kuliko sasa,na ndio haya sasa,tutakula nyasi km wanavyotukashifu kila kukicha na huyu chiligati sababu ni mueneza habari basi anaongea lolote tu,it' better to be silence and considered a fool,than speak out and remove all doubt,sasa huyu jamaa chiligati sasa kishanitoa doubt,sasa najua huyu jamaa ni chizi ambae anatumiwa na wachache kwa maslahi yao na si ya wananchi,huyo mwanyika nae nina wasiwasi na elimu yake,hv alisomea company law kweli au ndio vile vyeti kajanja tu magumashi utoto wa mjini,wakuu hapo juu wameeleza vizuri sana khs hizo pesa mi nafikiri watanzania sasa tunatukanwa kwa staili mpya ya kuja kuambiwa mambo ambayo watu wanayajua kuliko huyo anaeongea,ilibidi ajiulize pesa hz zinatoka wapi,au wakija kazini asubuhi wanazikuta zimeingia kwenye account tayari,ama vipi,mi naamini yale aliyosema makamba ya kua CCM ina miradi yake na inajitosheleza ndio hiyo deep green, au kuna mradi ambao wenzangu mnaujua ambao umewafanya CCM wapate pesanga zote zile za kampeni sitashangaa kuona wale wote wa rich-monduli,epa,na wengine wengi 2 wakitanua mtaani mpk watakapokufa na huyu ndio anaitwa rais makini,makini katika kulinda watu wanaokula nae,kwanza hakuta kitu kinachefua km kusema kikwete msafi,tokea lini huyu bwana akawa msafi au tuweke hadharani mambo yake,na najua tukiweka kuna wapuuzi wachache km asia atasema hizi siasa tu.

na mstari wa mbele, calif/usa, - 12.03.08 @ 19:06 | #1896

Bw.Chiligati na mtanzania mwenzangu Bujaga Izengo Kadago nyie wote lenu moja. Kadago tunajua wewe kama mtumishi wa serikali huwezi kuikosoa serikali ya CCM.Ni jambo ambalo haliingii akilini kwa mtu msomi kama wewe(hata kama bado unasoma huko saut)kusema kuwa tuwape muda mafisadi.Mwanyika na Hosea ni watuhumiwa wakubwa wa ufisadi, watawezaje kuwachunguza mafisadi wenzao?Kwa kutazama ripoti za tume mbalimbali zilizowahi kuundwa na kutolewa hadharani, ripoti ya Hosea wa takukuru ndio ripoti ya hovyo kuliko zote.Ndio maana sasahivi tunaamini kuwa takukuru haipambani na rushwa bali inaipamba!Kwa mtazamo huo huo hata ripoti ya mwisho itakayotolewa na mtu wetu IGP na washirika wa ufisadi TAKUKURU & AG inaonekana dhahiri kuwasafisha mafisadi. Haiingii akilini kutuambia eti pesa zinarudishwa lakini watu hawajulikani. Mlizoea kuwadanganya watanzania wa enzi zile, sio sasahivi.Kwakuwa rais wetu ameshindwa kuheshimu mawazo ya watanzania kufuatia ripoti ya kamati ya bunge iliyofichua waziwazi kuhusika kwa Hosea na Mwanyika katika ufisadi, basi lazima tuwe na mashaka na ukimya wa ris wetu, kwakuwa yeye ndiye tulimpa dhamana ya kutuongoza. Hivyo basi anapaswa kusimamia uadilifu kwa wateule wake. Kama Chiligati na Kadago mkiwa azalendo halisi mtakubaliana na watanzania wenzenu kuwa UFISADI sasa tosha, hakuna muda zaidi wa kuwapa.

na nyahende thomas, tz, - 12.03.08 @ 19:12 | #1897

Ni kweli kuna uhuni katika serikali ya Kikwete, nasema hivi kwa sababu ya hao watu wanaodaiwa kurudisha fedha zilizoibwa BoT kutokutajwa majina. Kama kweli Serikali iliyopo madarakani ina nia njema na nchi hii, inashindwaje kuchukua hatua dhidi ya hao wanaorudisha pesa zilizoibwa? Na kwa nini hao wanaorudisha pesa hawatajwi majina?. Au ndo tuseme na Jina la Mkuu wa nchi limo?

na Jamali Kileo, Tanzania, - 12.03.08 @ 19:13 | #1898

Kwa kweli sina imani na serikali iliyopo madarakani, sina imani na rais wala mawaziri wake. Mambo ambayo yamekuwa yakitokea, kwa serikali yoyote iliyo mstari wa mbele kutetea maslahi ya nchi, watu kama Lowassa wangeshafikishwa mahakamani, na hata Ubunge walionao hivi sasa, wangeshanyang'anywa. Lakini kwa kuwa Rais anawalinda watu hawa, basi hawawezi kupelekwa mbele ya sheria. Ndo maana hata amemteua Waziri mkuu ambaye hana maadili hata kidogo. Mizengo Pinda ni moja ya watu waliopata ubunge kwa njia za ulaghai (kule wilayani Mpanda, Rukwa) huyuhuyu Mizengo Pinda amekuwa akilalamikiwa na baadhi ya watu kwa vitendo vyake vya kihuni vya kuwajaza wanawake (wake) za watu mimba (uliza watu wa kule Mpanda, Rukwa watakwaqmbia). Sasa mtu kama huyu anapewa uongozi, nini tutegemee toka kwake?.

na moiza charls, Dar Es Salaam, Tanzania, - 12.03.08 @ 19:25 | #1901

Asia mnamuonea. Anaweza kuwa hawara wa CCM au wale matambara ya kudekia ya chama. Si unawajua wamejaa kweli kweli akina John Komba na manyang'au wengine waliouza roho na miili yao kwa ajili ya tumbo.
Wapo mbwa wala makombo akina Salva Rweyememu, Dr. Gideon Shoo na mbwa wengine wasio na mikia

na mbogo, kimanzichana Danganyika, - 12.03.08 @ 19:45 | #1902


Kutoka Tanzania Daima.



No comments: