Wednesday, March 12, 2008


Utapeli mpya waibuka Dar


Na Rachel Balama, Jijini

UTAPELI mpya umeibuka kwa wanawake kwa kutembea na vito bandia na kwenda sehemu zenye mikusanyiko ya wanawake wenzao kama saluni na kujifanya wanadaiwa PRIDE huku wakilia ili wapate fedha.

Mwandishi wa habari hizi, alishuhudia wanawake wakilizwa kwenye saluni moja jijini hapa pale alipofika mwanamke mmoja akiwa na vito vya dhahabu vinavyodaiwa kuwa ni bandia vya dhahabu.

Mama huyo ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja aliingia saluni hapo na vito hivyo huku akiwa anatokwa na machozi na kuwaeleza wanawake wenzake kuwa anadaiwa PRIDE hivyo ameamua kuuza ili akalipe.

Alidai kutokana na kudaiwa fedha nyingi PRIDE ameamua kuuza vito vyake vya dhahabu ili akalipe deni kitu ambacho kinadaiwa kuwa ni uongo.

Kutokana na baadhi ya wanawake waliokuwemo saluni walimuonea huruma dada huyo jinsi alivyokuwa akilia huku akiongea maneno ya huruma kila mmoja alianza kununua.

Hata hivyo mama huyo alipomalia kuwauzia vito hivyo aliwashukuru kwa kununua na kisha kuondoka zake.

Kutokana na shauku walizokuwa nazo wanawake hao kila mmoja alikuwa na shauku ya kutaka kujua zaidi mali waliyouziwa na mwanamke huyo na ndipo walipobaini kuwa ni dhahabu feki.

Baadhi ya wakazi wa jijini walioongea na Mwandishi wa Gazeti hili wameliomba Jeshi la Polisi kuendesha msako kuwasaka wanawake waliojiingiza katika uhalifu huo.

No comments: